Sunday, 27 December 2015

MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA MIKOPO WA SERIKALI ZA WANAFUNZI ZA VYUO VIKUU NCHINI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUWASILISHA MATATIZO YA WANAFUNZI KWA UONGOZI WA NCHI


Kikao cha umoja wa mawaziri  wa mikopo wa vyuo vikuu nchini, wamekutana leo katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kujadili namna ya kuwasilisha malalamiko yanayowakumba wanavyuo wanaopata mikopo kutoka bodi ya mikopo ya vyuo vikuu nchini.

Hali hii inafuatia, malalamiko mbalimbali yanayowakabili wanavyuo wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu nchini kukosa mikopo pamoja na kuwa na vigezo vinavyostahili, pamoja na wale wanaoendelea kucheleweshewa mikopo yao.

Kikao hicho kina lengo la kujenga hoja ya pamoja na kuwa na kauli moja wakati wa maandalizi  ya kuwasilisha matatizo yanayotokana na bodi ya mikopo nchini, kwa Mheshimiwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Majaliwa, katikati ya wiki ijayo.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), (aliyesimama) akitoa salam kwa mawaziri na manaibu mawaziri wa mikopo wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini waliohudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, kimehudhuriwa na mawaziri na manaibu mawaziri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini, na Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewakilishwa na Waziri wake wa mikopo Mheshimiwa Agrey Yaina pamoja na naibu wake Mheshimiwa Mkumbo.

Kushoto ni Mheshimiwa Mkumbo (naibu waziri wa mikopo) na waziri wake Mheshimiwa Agrey Yaina - waziri wa mikopo kutoka serikali ya wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii waliohudhuria katika kikao hicho.

Baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha leo, chenye lengo la kujenga hoja ya pamoja ya kutatua migogoro inayowakabili wanavyuo kutoka bodi ya mikopo na kupanga mkakati wa kuwasilisha matatizo hayo kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Continue Reading...

Saturday, 12 December 2015

MAHAFALI YA 39 CHUO CHA USTAWI WA JAMII YAFANA

Wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii waliomaliza mwaka wa masomo 2014/2015, wametakiwa kuchangamkia fursa za ajira zilizopo na pia kufikiria suala la kujiajiri wenyewe kwa kuwa wabunifu kwa kubuni miradi ya kimaendeleo.

Hayo yameelezwa leo katika mahafali ya 39 katika chuo cha ustawi wa jamii ambapo jumla ya wanachuo 1,053 wa ngazi mbalimbali wamehitimu katika mwaka wa masomo 2014/2015.

Idadi ya wahitimu kwa kila course ni kama ifuatavyo:-
DEPARTMENT OF SOCIAL WORKER

Bachelor Degree is Social Work - 141
Basic Technicians Certificate in Social Work - 138
Ordinary Diploma in Social Work - 205
Basic Technicians Certificate in Social Work - Kasangara Campus - 46.

DEPARTMENT OF HUMAN RESOURCES MANAGEMENT.
Bachelor Degree in Human Resource Management - 144
Ordinary Diploma in Human Resource Management - 136
Basic Technician Certificate in Human Resource Management - 85
Postgraduate  Diploma in Healthy System Management - 10
Postgraduate Diploma in Strategic Human Resource Management - 8

DEPARTMENT IN INDUSTRIAL RELATIONS
Bachelor Degree in Industrial Relations - 46
Certificate in Industrial Relations - 24
Diploma in Industrial Relations - 48
Higher Diploma in Industrial Relations - 1
Postgraduate Diploma in Industrial Relations - 21




Continue Reading...

Wednesday, 9 December 2015

NAIBU WAZIRI WA MAADILI - ISWOSO AONGOZA WANACHUO WANAOISHI HOSTEL YA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YANAYOZUNGUKA HOSTELI HIYO

Naibu waziri wa nidhamu na maadili wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO Mheshimiwa Hajrat Munisy, amewaongoza wanachuo wanaoishi hosteli ya taasisi kwa kufanya usafi wa mazingira, katika kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Naibu waziri wa nidhamu na maadili Mh. Hajrat Munisy (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya wanachuo wanaoishi hosteli ya taasisi ya ustawi wa jamii, wakiadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira.

Hatua hiyo ni kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Maghufuli ya kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanzania kwa mwaka huu, kwa kufanya usafi wa mazingira, ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ulioenea kwa kasi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.


Baadhi ya wanafunzi walijitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka hosteli hiyo, kufuatia mwamko walioupata kutoka kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO pamoja na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii.


Jengo la hostel wanaloishi wanachuo cha ustawi wa jamii, wakishiriki usafi kwa kuanzia vyumbani mwao na maeneo ya nje ya hosteli hiyo.
Continue Reading...

GLOBAL PEACE FOUNDATION - TANZANIA YAUNGANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI ISWOSO KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA TANZANIA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU

Shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Foundation limeungana na uongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO, na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Maghufuli, la kuadhimisha siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba kwa kufanya usafi wa mazingira, kupambana na ugonjwa wa kipindupindu. 


Mkurugenzi mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Foundation - Tanzania bi  Martha Ng'ambi (kulia) akiwa na mwakilishi wa shirika hilo Bi. Hilda Ngaja wakipozi baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.


Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo bi Martha Ng'ambi, asema amehamasika na namna vijana walivyojitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, kuitikia wito wa Mh. Rais na kwamba anaamini mpango huu utakuwa endelevu kwani wamepanga kushirikiana na uongozi wa serikali ya wanafunzi kuanzisha klabu ya vijana itakayohusianana mazingira.


Amebainisha kuwa, ingawa shirila lao linahusiana na amani, lakini pia wamelenga zaidi wanawake na watoto, kwa kuwa makundi haya ndiyo rahisi kushawishika katika kudumisha amani au kuibomoa.

Maadhimisho ya sherehe ya miaka 54 ya Uhuru mwaka huu yameadhimishwa nchini kote kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni jitahada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, ulioenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.




 Picha zote  ni baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO, na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii, wakati wa zoezi la usafi wa mazingira, kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.






























Continue Reading...
Continue Reading...

SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII - ISWOSO KWA KUSHIRIKIANA NA MENEJIMENT YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII YAADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YA CHUO

Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi ISWOSO (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii akiwemo mkuu wa idara ya Ustawi wa Jamii Leah Omari (wa tatu kutoka kulia), wakipozi baada ya kumaliza usafi wa maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira, kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kutumia siku ya maadhimisho ya uhuru wa Tanzania,  ya kufanya usafi wa mazingira kwa ujumla ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu, serikali ya wanafunzi ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii - ISWOSO ikiongozwa na makamu wa Rais wa serikali hiyo Mheshimiwa Stella Wadson, pamoja na menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii, wameshiriki kufanya usafi huo katika maeneo mbalimbali ya chuo cha ustawi wa jamii.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi -ISWOSO  (kushoto ) Mheshimiwa Stella Wadson akiwa na waziri wa elimu wa Mheshimiwa Mabena wakiendelea na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya chuo.

Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO walioshiri katika zoezi la usafi wa mazingira katika chuo cha ustawi wa jamii. Kutoka kushoto ni waziri mkuu Mh. Bendera,  waziri wa elimu Mh. Mabena, waziri wa Miundombinu Mh. Nassary na naibu waziri wa fedha Mh. Peace Nnauye. 

Pichani ni waziri wa afya na mazingira wa serikali ya wanafunzi ISWOSO Mh. Anderson Mahundi  (kushoto), na Mh. Victor. 



Baadhi ya viongozi wa ISWOSO walioshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira chuo cha ustawi wa jamii kufuatia agizo la rais wa Tanzania kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.


Continue Reading...

Thursday, 3 December 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU

Tanzania  imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya walemavu nchini ambapo tarehe 3 disemba ya kila mwaka imepangawa kuwa ni siku ya maadhimisho hayo.


Wakati hayo yakitokea suala la kujiuliza ni kuwa je miundo mbinu yetu hasa katika majengo ya serikali yanayotoa huduma za kijamii na hata yale ya binafsi, miundombinu yake ni rafiki kwa walemavu hao, je wanapewa kipaumbele gani katika kutetea haki zao, wanasikilizwa na je sera ya walemavu inatekelezeka ipasavyo.


Ni muda mrefu watu wenye ulemavu wa makundi yote wamekuwa wakilalamikia kutosikilizwa pamoja na kutotendewa haki stahiki, na wengine wakilalamikia usalama wa maisha yao (Albino), ni wakati sasa tushirikiane kwa pamoja katika kukumbushana kuhusiana utetezi wa haki za walemavu. Kwa mfano kwenye miundo mbinu ya usafiri, mtu mwenye ulemavu wa miguu anayetumia baiskeli hakuna mazingira yanayomwezesha kuingia na baiskeli yake, kama wenzetu wameweza naamini hata sisi pia tutaweza.

Tuungane kwa pamoja katika kutetea haki za wenzetu mimi na wewe.


Continue Reading...

Wednesday, 25 November 2015

MKUTANO WA KWANZA WA SERIKALI YA WANAFUNZI ISWOSO

Mkutano wa kwanza wa wanafunzi ISWOSO - STUDENTS GENERAL MEETING  ( SGM), unafanyika leo katika ukumbi wa chuo lengo kuu likiwa ni uzinduzi  wa katiba mpya ya serikali ya wanafunzi, pamoja na mashindano ya kitaaluma. 

Meza kuu

Katibu mkuu ofisi ya Rais - ISWOSO Mh.Victor Mutalemwa akitaka ufafanuzi wa vifungu vilivyoongezwa katika katiba mpya ya serikali ya wanafunzi.



Wanachuo wakifuatilia hotuba ya Rais akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi aliyoiahidi.
Continue Reading...

Monday, 23 November 2015

WELCOME FIRST YEAR FOR NEW INTAKE


Wizara ya Michezo na Burudani ISWOSO imeandaa bash ya aina yake kwa ajili ya kuwa kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza.

Karibu tujumuike pamoja kuwakaribisha wanachuo wenzetu. 
Continue Reading...

Thursday, 19 November 2015

MABORESHO YA VIMBWETA ISW 2015/2016 KUWEZESHA WANAFUNZI KUPATA MAHALI PA KUJISOMEA NYAKATI ZOTE

Katika kuendana na kasi ya mabadiliko katika suala la elimu vyuoni, uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii ISWOSO, kupitia wizara yake ya miundombinu imejipanga kufanya maboresho ya sehemu ya wanafunzi kujisomea (Vimbweta), kwa kuongeza idadi ili viweze kuongeza nafasi zaidi ya wanafunzi kupata sehemu za kujisomea.



Pichani ni Waziri wa Miundombinu ISWOSO 2016/2016 Mh. Erasto Nassary, akionesha sehemu ya vitendea kazi vinavyoendea kutengenezwa kwa ajili ya ujenzi wa vimbweta vipya. (picha zote ni kwa hisani ya wizara ya habari ISWOSO)

Ili kufanikisha suala hilo, wizara ya miundombinu katika serikali ya wanafunzi ISWOSO 2015/2016, imejipanga kuongeza idadi ya vimbweta zaidi ya ishirini baada ya jitihada za kupata ufadhili wa kufanikisha suala hilo kutoka asasi mbalimbali, huku kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL ikitoa mchango wake wa miamvuli 70 iliyoanza kuwekwa kwenye vimbweta vya awali ili wanafunzi waweze kujikinga na jua.




Pichani ni fundi akiendelea na maandalizi ya utengenezaji wa vimbweta vipya. 


Pichani juu ni baadhi ya vimbweta vya zamani vikiwa vimewekwa miamvuli iliyotolewa na Zantel kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kujikinga kipindi cha jua na manyunyu wakati wakijisomea.

Waziri wa Miundombinu ISWOSO 2015/2016 Mh. Nassary akiwa kwenye moja ya vimbweta vya awali vilivyowekwa miamvuli kwa hisani ya kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL.

Mh. Nassari, amebainisha kuwa vimbweta vinavyotarajiwa kutengenezwa vitakuwa kwa mtindo wa duara ili kuendana na sawa na umbo la miamvuli hiyo, na amewataka wanafunzi kutoondoa miamvuli hiyo sehemu ilipo na endapo atakaa kwenye kimbweta ambacho hakina mwamvuli afike ofisi za ISWOSO na kuelezea suala hilo kwani miamvuli mingine imehifadhiwa ofisini na si kuhamisha iliyowekwa kwenye vimbweta vingine.


NB: Shukran kwa kampuni ya Mawasiliano ya ZANTEL kwa msaada wa miamvuli

Continue Reading...

Wednesday, 18 November 2015

VIONGOZI WA KIMILA WAPITISHA AZIMIO LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE


Pichani  ni baahi ya viongozi wa kimila (Laigwanan na Laiboni) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan) wilayani Loliondo wakisoma na kujadili azimio la pamoja la kumlinda mtoto wa kila kabla ya kulipitisha na kusaini

Viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai na wanawake mashuhuri wilayani Ngorongoro, wamepitisha azimio la Loliondo lenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha maendeleo yake kiafya, kielimu na kiutamaduni.

Azimio hilo limetiwa sain na viongozi wa hao kwa hitimisho la kongomanao la siku mbili lililofanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, lililokuwa na lengo la kupinga mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike.

kabla ya kupitishwa na kusaini maazimio hayo, viongozi hao wakimila walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuendeleza mijadala na uelewa wa baadhi ya mila la desturi zinazochangia na kuchochea athari za kiafya na kijamii hasa kwa watoto wa kike na kina mama.

viongozi hao wa kimila (Laigwanan na Laibon) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan), kwa pamoja wamesema watatumia nafasi zao kuelimisha jamii juu ya malezi bora ikiwa ni pamoja na mahali salama pa kulala watoto wa kike na wa kiume na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu hasa kwa watoto wa kike.

Aidha wameiasa jamii ya kimaasai kuacha kuendelea na vitendo vya kuwaoza watoto wa kike wakiwa bado wadogo na wakati mwingine kuwakatisha masomo na kuwalazimisha kuolewa. 

Viongozi hao wamebainisha kuwa matukio ya vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni vimechangia utoro nyumbani na kwenda kuishi kwa muda kwenye vituo maalum kwa kuogopa kufanyiwa tohara na wamekuwa wakitoroka wapogundua kwamba kuna matukio ya ulemavu na athari nyinginezo za kiafyazinazotokana na ukeketaji na salama yao ni kujitoa katika jamii hiyo na kutafuta hifadhi kwingine.

Pamoja na utiani saini wa Azimio la Loliondo, viongozi hao wameliomba shirika la UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kushirikisha viongozi wengi zaidi, kuendelea kuwasaidia katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kuwasaidia uratibu wa shughuli zote za kupinga na unyanyasai wa kijinsia.

Kongamano hilo limeendeshwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi  na Utamaduni (UNESCO) limelenga kutoa elimu ya kuwajengea uwezo wa kugawa majukumu kwa viongozi wa kimila, wanawake mashuhuri, viongozi wa dini, wakunga wa jadi pamoja waandishi wa habari ili kutekeleza vizuri ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto katika jamii ya Kimaasai.
Continue Reading...

Wednesday, 4 November 2015

WANAWAKE WAJAWAZITO MANYONI WANAPOTEZA MAISHA KWA KUFUATA HUDUMA ZA AFYA UMBALI MREFU



IMEBAINIKA kuwa wanawake wajawazito wa Kijiji cha Maweni, wilayani Manyoni, Mkoani Singida wamekuwa wakipoteza maisha yao kutokana na umbali mrefu wanaoutumia kufuata huduma za afya ya uzazi kwa wakunga wa jadi.
Hali hii imetokana na kijiji hicho kutokuwa na kituo cha afya au zahanati kwa kipindi kirefu sasa huku ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho kutokamilika hali inayowalazimu kutembea zaidi ya kilomita kati ya 30 hadi 40 kufuata huduma hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa wananchi hao, Joyce Karikawe alisema kwa muda mrefu sasa akina mama wajazito hawana huduma za afya jambo linalowafanya watembee umbali mrefu kutoka katika Kijiji hicho hadi kwenye Hospitali ya misheni ya Kilimatinde umbali wa takribani kilomita zisizopungua 30.
Aidha Karikawe alifafanua kwamba pamoja na kufuata huduma hizo Kilimatinde lakini bado kuna baadhi yao wamekuwa wakienda kujifungulia kwa wakunga wa jadi waliopo kwenye maeneo ya kata hiyo,ambayo hata hivyo hupata matatizo makubwa sana,ikiwemo kupoteza maisha yao.
Kutokana na adha hiyo inayowapata wanawake na wananchi kwa ujumla wa kijiji hicho,Karikawe alibainisha kwamba kumewalazimu kufikia maamuzi ya kujenga zahanati katika Kijiji hicho itakayowawezesha kukabiliana na vifo vya akina mama wajawazito vinavyotokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Naye mkazi wa Kijiji cha Maweni, Jacobo Jacksoni Karikawe alifafanua kuwa tatizo la kukosekana kwa zahanati katika Kijiji hicho ni la muda mrefu tangu nchi ilipopata uhuru wake,lakini kutokana na jitihada za diwani wao waliomchagua mwaka 2010 hadi 2015, aliwaonyesha moyo na kuwatia nguvu hadi wameweza kuinua jengo hilo la zahanati.
SAM_0153.jpg
Jengo la zahanati inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo itakapokamilika inatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja.
“Lakini jengo hili bado halijakamilika, jengo hili tunaomba msaada kutoka serikalini kwa sababu kuna akina mama wanatoka umbali wa kilomita 15 hadi 20 wanapata matatizo wengine wanajifungulia njiani”alisisitiza Karikawe.
Hivyo mwanachi huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa kuchaguliwa kutosahau ahadi wanazowaahidi wananchi wakati wa kampeni za auchaguzi ili waweze kurejesha imani kwa serikali na kuonya kwamba kutotekelezwa kwa ahadi kunachangia wananchi kutokuwa na imanai na vyama vya siasa wakati wa kuomba kura.
Kwa upande wake Yustasi Wilsoni Mahajile aliweka bayana kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu imekuwa vigumu kwao kukutana na vidonge Kijijini hapo,zaidi ya kwenda kuvifuata kwenye vijiji jirani cha Mvumi,Kintinku hali inayochangia magonjwa ya milipuko pamoja na idadi kubwa ya wagonjwa kupoteza maisha yao.
“Yaani ukishakosa huduma ya afya ina maana magonjwa ya milipuko yanaweza yakatokea na wallio wengi tunakufa,halafu yaani unapokosa dawa ina maana kwamba unatarajia kifo kwa hivyo ukipata zahanati itakuwa ni kimbilio la kuweza kupata maisha pale”alifafanua. 
Hata hivyo kwa upande wake aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye pia ameshinda katika uchaguzi uliofanyika okt, 25,mwaka huu, Abduli Mwengwa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016 Halmashauri ya wilaya ya Manyoni imetenga zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho.
Kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji cha Maweni,Merina Nyambuya alisema ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho ulioanza mwaka 2012 kwa nguvu za wananchi unatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja utakapokamilika na kwamba mpaka sasa lilipofikia hatua ya umaliziaji limetumia zaidi ya shilingi milioni 41.

NB: Shukran Zainul Mzige wa Moblog
Continue Reading...

Monday, 12 October 2015

TAMASHA LA MTOTO WA KIKE LAFANA NA LATOA KAULI NZITO


WAKATI serikali imekiri kwamba pamoja na kuwa na sheria kali za kuzuia ukatili kwa watoto bado kuna matukio mengi yanayowanyima watoto uhuru na haki zao msingi,wadau mbalimbali walioshiriki tamasha la mtoto msichana wamewataka wasichana kutimiza ndoto zao.
Katika tamasha hilo lililofanyika katika shule ya msingi Tandale, wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane vipaji mbalimbali vya watoto vilioneshwa na watoto nao kutoa kauli zao za kutaka haki na ustawi wao kwani wao ni taifa la sasa.
DSC_0486.JPG.jpg

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe Mussai akiwaasa watoto wa kike kuzingatia elimu kwani ndio nguzo ya msingi katika maisha yao wakati w siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Tandale jijini Dar.

Pamoja na watoto hao kutoa ushuhuda na kuonesha njia ya kusaidiwa, Mkurugenzi wa watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii , jinsia na watoto Margaret Sawe Mussai pamoja na kuwaambia watoto na jamii kutumia simu 119  kuelezea ukatili, ametaka madawati yaliyopo Polisi kutumika vilivyo kukabiliana na vitendo hivyo.
Alisema lazima wazazi na walezi wawajibike katika kulinda watoto kwani taarifa zilizopo sasa haziridhishi hata kidogo.
Alisema taarifa zilizopo watoto wa kike asilimia 29 na wavulana asilimia 13 wamenyanyaswa kijinsia wakati wasichana asilimia 14 na wavulana asilimia 6 wamekabiliwa na tatizo la kujaribiwa kuvurugwa kijinsia.


DSC_0418.JPG.jpg


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar.

Akizungumzia suala la mimba za utotoni alisema kwamba wizara imeandaa program za kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni huku akisema kwamba sheria ya ndoa ya mwaka 1971 iko mbioni kubadilishwa ili kupandisha umri wa kuolewa kuwa miaka 18.
Aidha alisema serikali na wadau wengine wanaendesha mafunzo ya kuwatoa watoto katika mazingira hatarishi pamoja na kusaidia wazazi vijana ambao walikatisha shule kutokana na ujauzito.
Mkurugenzi huyo pamoja na kueleza changamoto za malezi na ulinzi kwa watoto amesema sera zilizopo zinaendelea kuboreshwa ili kutoa ulinzi zaidi katika kuhakikisha taifa linakua na watoto wenye uhakika wa usalama.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu UNFPA Dk. Natalia Kanem alisema mtoto msichana anahitaji kushikilia ndoto yake pamoja na changamoto zinazojitokeza.
Alisema pamoja na kuwepo kwa vikwazo vya mawasiliano , mtoto wa kike anastahili kupewa taarifa mbalimbali zinazomweka huru katika mambo ambayo yanamhusu yeye na jamii yake.
Alisema pamoja na haja ya kuwepo kwa usawa wa kijinsia, mtoto wa kike ni lazima apate haki yake ya kusoma,kutodhuriwa na utamaduni uliopitwa na wakati ambao ni kandamizi kama kukeketwa na ndoa za utotoni na kutobaguliwa.

DSC_0309.JPG.jpg


Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisoma risala kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar

Aliwataka watoto wa kike kuhakikisha kwamba wanasoma kwa kuwa elimu ni kila kitu na wakishakuwa na elimu watajiamini na kujitambua.
Alisema ipo haja ya kuimarisha mfumo wa ulinzi kwa watoto wa kike ili  kupata nafasi ya kusonga mbele na wale ambao wamekatishwa masomo kwa sababu mbalimbali kurejea darasani ili kupata elimu na uwezo wa kuendelea mbele.
Alisema kw akuunganisha nguvu kati ya serikali, mashirika ya umoja wa mataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo na mtoto wa kike,watoto wa kike watapata nafasi kubwa ya kusonge mbele.
Aliwataka watoto wa kike kujitambua kwamba wao ni wazuri lakini wanapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo yao.
“Wale wanaoapata mimba, wale wanaokatishwa masomo ni lazima wapate njia ya kujiendeleza tena” alisema Dk Natalia.
DSC_0343.JPG.jpg

Angel Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani akieleza alipotokea mpaka kufika alipo sasa wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika siku ya Jumamosi.
Katika tamasha hilo wasichana wawili walitoa ushuhuda, Binti mdogo Eva Tolage ambaye alimwandikia barua Rais Barak Obama akihoji Marekani na yeye binafsi rais Obama na viongozi wa dunia watafanya nini kumsaidia mtoto wa kike anayekabiliwa na changamoto nyingi hasa wale wa vijijini.
Eva alimwambia Barack Obama kwamba anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa askari kusaidia jamii, lakini atafikiaje ndoto hiyo wakati kuna changamoto ya umeme na huku baba yake kazi anazofanya hazimpi kipato cha kutosha.
Msichana huyo ambaye aliandika barua kwa ujasiri mkubwa akihoji maendeleo endelevu yasiyompita binti mdogo alijibiwa na Rais Obama na kutajwa katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa kwamba viongozi wa dunia akiwemo Barack Obama mwenyewe wamemsikia na watahakikisha tatizo la wasichana wa Afrika na kwingine kokote linaondolewa na na wanapata nafasi ya kushiriki katika maendeleo.
DSC_0362.JPG.jpg

Eva Tolage aliyeandika barua kwa rais Barack Obama wa Marekani na barua yake kusomwa katika mkutano wa viongozi wa dunia makao makuu ya Umoja wa Mataifa alitumia mkutano huo kusoma machache aliyoandika. Katika barua hiyo, Eva mwenye umri wa miaka 15, alielezea jinsi ambavyo bado mazingira mtoto ni mabovu na hatarishi kiasi cha kumfanya ashindwe kupata elimu bora, pia kuwa katika hatari ya kukumbwa na vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Aidha binti mwingine Angela Benedicto ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wote sawa alisimulia  matatizo ya wasichana wa kazi,adha zao kutoka kwa wanaume na watoto wa kiume wanakofanyia kazi.
Alisema kwamba mateso wanayoyapata wasichana wa kazi yanastahili kukoma na kwamba ipo haja ya kuwekwa kwa mfumo unawalinda.
Alisema serikali ina wajibu wa kuwatetea wasichana kupata haki zao, sio tu kusema shule bure, lakini pia kujenga kujiamini kwa wasichana katika kutimiza ndoto zao.
Alisema sababu za kuwepo kwa wasichana wengi wakazi za ndani ni dhuluma inayoambatana na umaskini katika familia na tamaduni zinazomweka nyuma mtoto wa kike kiasi cha kulazimika kutafuta kazi za ndani ambazo waajiri wanakuwa hawana staha.
Katika tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za kuangalia hali ya afya ya uzazi, elimu ya afya ya uzazi, kupimwa maambukizi ya UKIMWI na kukaguliwa kwa saratani ya matiti na kizazi pamoja na elimu yake.
Pia kulikuwa na michezo ya kuigiza na sarakasi na mwanamuziki wa kike mwasiti alichombeza kwa nyimbo zake za uadilifu.
Siku ya Mssichana duniani huadhimkishwa Oktoba 11 lakini kwa Tanzania iliadhimishwa Oktoba 10.

DSC_0751.JPG.jpg

Mgeni rasmi pamoja na vingozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wenye ulemavu wa ngozi katoka maadhimisho ya siku wa mtoto wa kike.
DSC_0750.JPG.jpg


Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe Mussai (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem ( wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na watoa huduma katika mabanda yaliyokuwepo kwenye maadhimisho hayo.


Continue Reading...

Friday, 9 October 2015

Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kufanyika Octoba 13 viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar


Kila Oktoba 24 ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kuundwa kwake. Kwa mwaka huu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yanayofanya kazi kama taasisi moja yameendelea kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo.

Akizungumza  na waandishi wa habari Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez kuhusu  umuhimu wa  malengo hayo  amesema “Kwa hakika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni wito wa kujitazama, kuona yale tuliyofanya kwa miongo kadhaa na kujikita kuona namna  ya kuabiliana na umaskini hapa nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla
DSC_0162.JPG.jpg

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.
DSC_0181.jpg

Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa  kwa Umoja wa Mataifa yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
“Malengo ya Maendeleo endelevu ni wito wa kuwajibika kwetu sote.  Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake.  Inabidi tufanye kazi kwa pamoja,wadau wote,serikali na bunge, vyama vya kiraia, madhehebu ya kidini, wafanya biashara, wajasiliamali, na wanazuoni.Na hakika tukishirikiana kwa nguvu pamoja na amani tunaweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu”
Pia alisistiza kuwa “Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumzana waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya amesema kuwa nia ya serikali ni kuendelea kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na kuwatakawatengeneze sera nzuri ambazio zitahakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mipango ya maendeleo ya kitaifa.
DSC_0174.JPG.jpg
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni.

Aliendelea kufafanua kwa kusema Tanzania inafurahishwa na ukweli unaoonekana kwenye malengo mapya ya maendeleo endelevu kwani  yamechota pia yale malengo ya milenia ambayo yalikuwa bado hayajamaliziwa kwani katika hayo kunaweza kuleta mabadiliko ya kuwezesha kuondokanana umaskini katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya Umoja wa mataifa yatafavyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne Oktoba 13 badala ya siku iliyozoelekaya Oktoba 24 ili kupisha uchaguzi mkuu wa  Tanzania unaofanyika Oktoba 25. Na kauli mbiu ya maadhimisho ya Umoja wa mataifa mwaka huu ni “Umoja wa Mataifa uliothabiti, Dunia bora”.
DSC_0048.JPG.jpg

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0071.JPG.jpg

Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo namba 4 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0023.JPG.jpg

Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wameshikilia lengo namba 5 na 10 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0085.JPG.jpg

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiwa ameshikilia lengo namba 17 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0120.JPG.jpg

Afisa Habari wa Shirika la kazi duniani (ILO)  Tanzania, Magnus Minja na Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakiwakilisha lengo namba 1 na 8.

NB: Shukran Pamoja Blog na Mo Blog kwa kufanikisha habari hii.


Continue Reading...

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia