Sunday, 27 December 2015

MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA MIKOPO WA SERIKALI ZA WANAFUNZI ZA VYUO VIKUU NCHINI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUWASILISHA MATATIZO YA WANAFUNZI KWA UONGOZI WA NCHI

Share it Please

Kikao cha umoja wa mawaziri  wa mikopo wa vyuo vikuu nchini, wamekutana leo katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kujadili namna ya kuwasilisha malalamiko yanayowakumba wanavyuo wanaopata mikopo kutoka bodi ya mikopo ya vyuo vikuu nchini.

Hali hii inafuatia, malalamiko mbalimbali yanayowakabili wanavyuo wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu nchini kukosa mikopo pamoja na kuwa na vigezo vinavyostahili, pamoja na wale wanaoendelea kucheleweshewa mikopo yao.

Kikao hicho kina lengo la kujenga hoja ya pamoja na kuwa na kauli moja wakati wa maandalizi  ya kuwasilisha matatizo yanayotokana na bodi ya mikopo nchini, kwa Mheshimiwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Majaliwa, katikati ya wiki ijayo.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), (aliyesimama) akitoa salam kwa mawaziri na manaibu mawaziri wa mikopo wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini waliohudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, kimehudhuriwa na mawaziri na manaibu mawaziri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini, na Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewakilishwa na Waziri wake wa mikopo Mheshimiwa Agrey Yaina pamoja na naibu wake Mheshimiwa Mkumbo.

Kushoto ni Mheshimiwa Mkumbo (naibu waziri wa mikopo) na waziri wake Mheshimiwa Agrey Yaina - waziri wa mikopo kutoka serikali ya wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii waliohudhuria katika kikao hicho.

Baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha leo, chenye lengo la kujenga hoja ya pamoja ya kutatua migogoro inayowakabili wanavyuo kutoka bodi ya mikopo na kupanga mkakati wa kuwasilisha matatizo hayo kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

No comments:

Post a Comment

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia