Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya walemavu nchini ambapo tarehe 3 disemba ya kila mwaka imepangawa kuwa ni siku ya maadhimisho hayo.
Wakati hayo yakitokea suala la kujiuliza ni kuwa je miundo mbinu yetu hasa katika majengo ya serikali yanayotoa huduma za kijamii na hata yale ya binafsi, miundombinu yake ni rafiki kwa walemavu hao, je wanapewa kipaumbele gani katika kutetea haki zao, wanasikilizwa na je sera ya walemavu inatekelezeka ipasavyo.
Ni muda mrefu watu wenye ulemavu wa makundi yote wamekuwa wakilalamikia kutosikilizwa pamoja na kutotendewa haki stahiki, na wengine wakilalamikia usalama wa maisha yao (Albino), ni wakati sasa tushirikiane kwa pamoja katika kukumbushana kuhusiana utetezi wa haki za walemavu. Kwa mfano kwenye miundo mbinu ya usafiri, mtu mwenye ulemavu wa miguu anayetumia baiskeli hakuna mazingira yanayomwezesha kuingia na baiskeli yake, kama wenzetu wameweza naamini hata sisi pia tutaweza.
Tuungane kwa pamoja katika kutetea haki za wenzetu mimi na wewe.
No comments:
Post a Comment