Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi ISWOSO (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii akiwemo mkuu wa idara ya Ustawi wa Jamii Leah Omari (wa tatu kutoka kulia), wakipozi baada ya kumaliza usafi wa maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira, kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.
Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kutumia siku ya maadhimisho ya uhuru wa Tanzania, ya kufanya usafi wa mazingira kwa ujumla ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu, serikali ya wanafunzi ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii - ISWOSO ikiongozwa na makamu wa Rais wa serikali hiyo Mheshimiwa Stella Wadson, pamoja na menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii, wameshiriki kufanya usafi huo katika maeneo mbalimbali ya chuo cha ustawi wa jamii.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi -ISWOSO (kushoto ) Mheshimiwa Stella Wadson akiwa na waziri wa elimu wa Mheshimiwa Mabena wakiendelea na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya chuo.
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO walioshiri katika zoezi la usafi wa mazingira katika chuo cha ustawi wa jamii. Kutoka kushoto ni waziri mkuu Mh. Bendera, waziri wa elimu Mh. Mabena, waziri wa Miundombinu Mh. Nassary na naibu waziri wa fedha Mh. Peace Nnauye.
Pichani ni waziri wa afya na mazingira wa serikali ya wanafunzi ISWOSO Mh. Anderson Mahundi (kushoto), na Mh. Victor.
No comments:
Post a Comment