Mkurugenzi mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Foundation - Tanzania bi Martha Ng'ambi (kulia) akiwa na mwakilishi wa shirika hilo Bi. Hilda Ngaja wakipozi baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.
Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo bi Martha Ng'ambi, asema amehamasika na namna vijana walivyojitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, kuitikia wito wa Mh. Rais na kwamba anaamini mpango huu utakuwa endelevu kwani wamepanga kushirikiana na uongozi wa serikali ya wanafunzi kuanzisha klabu ya vijana itakayohusianana mazingira.
Amebainisha kuwa, ingawa shirila lao linahusiana na amani, lakini pia wamelenga zaidi wanawake na watoto, kwa kuwa makundi haya ndiyo rahisi kushawishika katika kudumisha amani au kuibomoa.
Maadhimisho ya sherehe ya miaka 54 ya Uhuru mwaka huu yameadhimishwa nchini kote kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni jitahada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, ulioenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.
Picha zote ni baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO, na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii, wakati wa zoezi la usafi wa mazingira, kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment