Pichani ni baahi ya viongozi wa kimila (Laigwanan na Laiboni) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan) wilayani Loliondo wakisoma na kujadili azimio la pamoja la kumlinda mtoto wa kila kabla ya kulipitisha na kusaini.
Viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai na wanawake mashuhuri wilayani Ngorongoro, wamepitisha azimio la Loliondo lenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha maendeleo yake kiafya, kielimu na kiutamaduni.
Azimio hilo limetiwa sain na viongozi wa hao kwa hitimisho la kongomanao la siku mbili lililofanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, lililokuwa na lengo la kupinga mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike.
kabla ya kupitishwa na kusaini maazimio hayo, viongozi hao wakimila walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuendeleza mijadala na uelewa wa baadhi ya mila la desturi zinazochangia na kuchochea athari za kiafya na kijamii hasa kwa watoto wa kike na kina mama.
viongozi hao wa kimila (Laigwanan na Laibon) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan), kwa pamoja wamesema watatumia nafasi zao kuelimisha jamii juu ya malezi bora ikiwa ni pamoja na mahali salama pa kulala watoto wa kike na wa kiume na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu hasa kwa watoto wa kike.
Aidha wameiasa jamii ya kimaasai kuacha kuendelea na vitendo vya kuwaoza watoto wa kike wakiwa bado wadogo na wakati mwingine kuwakatisha masomo na kuwalazimisha kuolewa.
Viongozi hao wamebainisha kuwa matukio ya vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni vimechangia utoro nyumbani na kwenda kuishi kwa muda kwenye vituo maalum kwa kuogopa kufanyiwa tohara na wamekuwa wakitoroka wapogundua kwamba kuna matukio ya ulemavu na athari nyinginezo za kiafyazinazotokana na ukeketaji na salama yao ni kujitoa katika jamii hiyo na kutafuta hifadhi kwingine.
Pamoja na utiani saini wa Azimio la Loliondo, viongozi hao wameliomba shirika la UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kushirikisha viongozi wengi zaidi, kuendelea kuwasaidia katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kuwasaidia uratibu wa shughuli zote za kupinga na unyanyasai wa kijinsia.
Kongamano hilo limeendeshwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limelenga kutoa elimu ya kuwajengea uwezo wa kugawa majukumu kwa viongozi wa kimila, wanawake mashuhuri, viongozi wa dini, wakunga wa jadi pamoja waandishi wa habari ili kutekeleza vizuri ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto katika jamii ya Kimaasai.
No comments:
Post a Comment