Sunday, 27 December 2015

MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA MIKOPO WA SERIKALI ZA WANAFUNZI ZA VYUO VIKUU NCHINI WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUWASILISHA MATATIZO YA WANAFUNZI KWA UONGOZI WA NCHI


Kikao cha umoja wa mawaziri  wa mikopo wa vyuo vikuu nchini, wamekutana leo katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), kujadili namna ya kuwasilisha malalamiko yanayowakumba wanavyuo wanaopata mikopo kutoka bodi ya mikopo ya vyuo vikuu nchini.

Hali hii inafuatia, malalamiko mbalimbali yanayowakabili wanavyuo wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu nchini kukosa mikopo pamoja na kuwa na vigezo vinavyostahili, pamoja na wale wanaoendelea kucheleweshewa mikopo yao.

Kikao hicho kina lengo la kujenga hoja ya pamoja na kuwa na kauli moja wakati wa maandalizi  ya kuwasilisha matatizo yanayotokana na bodi ya mikopo nchini, kwa Mheshimiwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Majaliwa, katikati ya wiki ijayo.

Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), (aliyesimama) akitoa salam kwa mawaziri na manaibu mawaziri wa mikopo wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini waliohudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, kimehudhuriwa na mawaziri na manaibu mawaziri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini, na Taasisi ya Ustawi wa Jamii imewakilishwa na Waziri wake wa mikopo Mheshimiwa Agrey Yaina pamoja na naibu wake Mheshimiwa Mkumbo.

Kushoto ni Mheshimiwa Mkumbo (naibu waziri wa mikopo) na waziri wake Mheshimiwa Agrey Yaina - waziri wa mikopo kutoka serikali ya wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii waliohudhuria katika kikao hicho.

Baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wa serikali ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha leo, chenye lengo la kujenga hoja ya pamoja ya kutatua migogoro inayowakabili wanavyuo kutoka bodi ya mikopo na kupanga mkakati wa kuwasilisha matatizo hayo kwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Continue Reading...

Saturday, 12 December 2015

MAHAFALI YA 39 CHUO CHA USTAWI WA JAMII YAFANA

Wahitimu wa chuo cha ustawi wa jamii waliomaliza mwaka wa masomo 2014/2015, wametakiwa kuchangamkia fursa za ajira zilizopo na pia kufikiria suala la kujiajiri wenyewe kwa kuwa wabunifu kwa kubuni miradi ya kimaendeleo.

Hayo yameelezwa leo katika mahafali ya 39 katika chuo cha ustawi wa jamii ambapo jumla ya wanachuo 1,053 wa ngazi mbalimbali wamehitimu katika mwaka wa masomo 2014/2015.

Idadi ya wahitimu kwa kila course ni kama ifuatavyo:-
DEPARTMENT OF SOCIAL WORKER

Bachelor Degree is Social Work - 141
Basic Technicians Certificate in Social Work - 138
Ordinary Diploma in Social Work - 205
Basic Technicians Certificate in Social Work - Kasangara Campus - 46.

DEPARTMENT OF HUMAN RESOURCES MANAGEMENT.
Bachelor Degree in Human Resource Management - 144
Ordinary Diploma in Human Resource Management - 136
Basic Technician Certificate in Human Resource Management - 85
Postgraduate  Diploma in Healthy System Management - 10
Postgraduate Diploma in Strategic Human Resource Management - 8

DEPARTMENT IN INDUSTRIAL RELATIONS
Bachelor Degree in Industrial Relations - 46
Certificate in Industrial Relations - 24
Diploma in Industrial Relations - 48
Higher Diploma in Industrial Relations - 1
Postgraduate Diploma in Industrial Relations - 21




Continue Reading...

Wednesday, 9 December 2015

NAIBU WAZIRI WA MAADILI - ISWOSO AONGOZA WANACHUO WANAOISHI HOSTEL YA TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YANAYOZUNGUKA HOSTELI HIYO

Naibu waziri wa nidhamu na maadili wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO Mheshimiwa Hajrat Munisy, amewaongoza wanachuo wanaoishi hosteli ya taasisi kwa kufanya usafi wa mazingira, katika kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Naibu waziri wa nidhamu na maadili Mh. Hajrat Munisy (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya wanachuo wanaoishi hosteli ya taasisi ya ustawi wa jamii, wakiadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira.

Hatua hiyo ni kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Maghufuli ya kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanzania kwa mwaka huu, kwa kufanya usafi wa mazingira, ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ulioenea kwa kasi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.


Baadhi ya wanafunzi walijitokeza kwa wingi kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka hosteli hiyo, kufuatia mwamko walioupata kutoka kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO pamoja na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii.


Jengo la hostel wanaloishi wanachuo cha ustawi wa jamii, wakishiriki usafi kwa kuanzia vyumbani mwao na maeneo ya nje ya hosteli hiyo.
Continue Reading...

GLOBAL PEACE FOUNDATION - TANZANIA YAUNGANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI ISWOSO KUADHIMISHA SIKU YA UHURU WA TANZANIA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU

Shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Foundation limeungana na uongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO, na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Maghufuli, la kuadhimisha siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba kwa kufanya usafi wa mazingira, kupambana na ugonjwa wa kipindupindu. 


Mkurugenzi mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Global Peace Foundation - Tanzania bi  Martha Ng'ambi (kulia) akiwa na mwakilishi wa shirika hilo Bi. Hilda Ngaja wakipozi baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.


Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo bi Martha Ng'ambi, asema amehamasika na namna vijana walivyojitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, kuitikia wito wa Mh. Rais na kwamba anaamini mpango huu utakuwa endelevu kwani wamepanga kushirikiana na uongozi wa serikali ya wanafunzi kuanzisha klabu ya vijana itakayohusianana mazingira.


Amebainisha kuwa, ingawa shirila lao linahusiana na amani, lakini pia wamelenga zaidi wanawake na watoto, kwa kuwa makundi haya ndiyo rahisi kushawishika katika kudumisha amani au kuibomoa.

Maadhimisho ya sherehe ya miaka 54 ya Uhuru mwaka huu yameadhimishwa nchini kote kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni jitahada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ya kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, ulioenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.




 Picha zote  ni baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO, na menejiment ya uongozi wa chuo cha ustawi wa jamii, wakati wa zoezi la usafi wa mazingira, kuadhimisha siku ya uhuru wa Tanzania.






























Continue Reading...
Continue Reading...

SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII - ISWOSO KWA KUSHIRIKIANA NA MENEJIMENT YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII YAADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YA CHUO

Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi ISWOSO (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii akiwemo mkuu wa idara ya Ustawi wa Jamii Leah Omari (wa tatu kutoka kulia), wakipozi baada ya kumaliza usafi wa maeneo ya chuo cha ustawi wa jamii, katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira, kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kutumia siku ya maadhimisho ya uhuru wa Tanzania,  ya kufanya usafi wa mazingira kwa ujumla ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu, serikali ya wanafunzi ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii - ISWOSO ikiongozwa na makamu wa Rais wa serikali hiyo Mheshimiwa Stella Wadson, pamoja na menejiment ya chuo cha ustawi wa jamii, wameshiriki kufanya usafi huo katika maeneo mbalimbali ya chuo cha ustawi wa jamii.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi -ISWOSO  (kushoto ) Mheshimiwa Stella Wadson akiwa na waziri wa elimu wa Mheshimiwa Mabena wakiendelea na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya chuo.

Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi ISWOSO walioshiri katika zoezi la usafi wa mazingira katika chuo cha ustawi wa jamii. Kutoka kushoto ni waziri mkuu Mh. Bendera,  waziri wa elimu Mh. Mabena, waziri wa Miundombinu Mh. Nassary na naibu waziri wa fedha Mh. Peace Nnauye. 

Pichani ni waziri wa afya na mazingira wa serikali ya wanafunzi ISWOSO Mh. Anderson Mahundi  (kushoto), na Mh. Victor. 



Baadhi ya viongozi wa ISWOSO walioshiriki katika zoezi la usafi wa mazingira chuo cha ustawi wa jamii kufuatia agizo la rais wa Tanzania kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi wa mazingira kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.


Continue Reading...

Thursday, 3 December 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA WALEMAVU

Tanzania  imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya walemavu nchini ambapo tarehe 3 disemba ya kila mwaka imepangawa kuwa ni siku ya maadhimisho hayo.


Wakati hayo yakitokea suala la kujiuliza ni kuwa je miundo mbinu yetu hasa katika majengo ya serikali yanayotoa huduma za kijamii na hata yale ya binafsi, miundombinu yake ni rafiki kwa walemavu hao, je wanapewa kipaumbele gani katika kutetea haki zao, wanasikilizwa na je sera ya walemavu inatekelezeka ipasavyo.


Ni muda mrefu watu wenye ulemavu wa makundi yote wamekuwa wakilalamikia kutosikilizwa pamoja na kutotendewa haki stahiki, na wengine wakilalamikia usalama wa maisha yao (Albino), ni wakati sasa tushirikiane kwa pamoja katika kukumbushana kuhusiana utetezi wa haki za walemavu. Kwa mfano kwenye miundo mbinu ya usafiri, mtu mwenye ulemavu wa miguu anayetumia baiskeli hakuna mazingira yanayomwezesha kuingia na baiskeli yake, kama wenzetu wameweza naamini hata sisi pia tutaweza.

Tuungane kwa pamoja katika kutetea haki za wenzetu mimi na wewe.


Continue Reading...

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia