Friday, 13 May 2016

PATA VIONJO - YALIYOJIRI KWENYE CAREER DAY USTAWI WA JAMII

Share it Please
Katika kunogesha maadhimisho ya siku ya ujuzi (Career day) yaliyofanyika jana alhamisi ya tarehe 12/05/2016, vikundi mbalimbali vya kitaaluma vilitoa burudani inayohusiana na kile wanachojifunza katika taaluma yao.

Kwa upande wa taaluma ya Social work, wanaharakati wa kikundi cha Protect Her 4 Life, chenye lengo la kupambana na kila aina ya ukatili wanaofanyiwa wanawake na wasichana, kilitoa igizo lililolenga namna ukatili unavyofanyika, ni kwa kiasi gani kutojielewa au kutojengewa uwezo kunavyosababisha mtu kutoweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo, namna mwanamume anayomtupia lawama mke kwa kila tatizo linalomkuta mtoto na kuelimishwa kuwa naye anapaswa kuwa sehemu ya kutoa malezi bora kwa watoto.

Pia igizo hilo lilionesha ni kwa namna gani afisa ustawi wa jamii anavyoweza kufanya kazi na timu ya wataalamu wa fani mbalimbali, na katika igizo hili wameshirikiana na polisi kufanikisha mwanamume aliyefanya ukatili amekamatwa na kufikishwa dawati la jinsia, pia afisa ustawi wa jamii ameweza kushirikiana na mwalimu wa shule katika kusaidiana kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana hasa kipindi cha balehe ili kuepuka mimba wakiwa mashuleni na kuonesha ni kwa kiasi gani maafisa ustawi wa jamii wahahitajika mashuleni. Na pia kumjengea uwezo mwanamke afahamu haki zake na fursa mbalimbali za kimaendeleo.



Wanachuo wa fani ya ustawi wakijiandaa kwa igizo

Mwanamke aliyepigwa na mumewe akishauriwa kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi, kutokana na kipigo cha mara kwa mara anachokipata kwa mumewe.





Msoma risala kwa upande wa Industrial Relations wao hawakuwa na igizo.





No comments:

Post a Comment

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia