Wizara ya elimu kupitia serikali ya wanafunzi ya
chuo cha ustawi wa jamii – Institute of Social Work Students Organization ISWOSO kwa kushirikiana na club za
vitengo vinavyotoa taaluma chuoni hapa, wameandaa maadhimisho ya siku ya ujuzi
maarufu kama CAREER DAY yenye lengo la kuwakutanisha wataalamu mbalimbali
waliosoma chuoni hapo wa fani tofauti kuanzia leo tarehe 9 hadi 12 mwezi huu wa
tano, 2016.
Maadhimisho hayo ya Career day yanashirikisha
wataalamu na wanachuo kutoka taaluma ya Rasilimali watu (Human Resource
Management), Mahusiano kazini (Industrial Relations) na Ustawi wa jamii (Social
work).
Akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha
Taifa – TBC mwishoni mwa wiki, waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha
ustawi wa jamii mheshimiwa Maurice Bendera, amewaomba wanafunzi kutoka vyuo
mbalimbali kushiriki katika wiki hii kwani kuna mambo mengi ambayo yameandaliwa
na wanachuo.
Ametaja baadhi ya mambo yatakayokuwa yakiendelea
katika wiki hii ujuzi ni pamoja na Huduma ya unasihi (Counseling) ikayokuwa
ikitolewa na wanachuo, elimu kwa upande wa labour studies kwani imeonekana
wafanyakazi wengi hawafahamu sheria mbalimbali zinazowaongoza na ili kutambua
haki zao kutoka kwa mwajiri, pamoja na maafisa rasilimali watu ambao watatoa
elimu kuhusiana na sheria za kazi (Employment Labour Relations Act), na
kuwakaribisha wanafunzi wote na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu kwani
huduma hii inatolewa bure.
Siku ya jumatano imetengwa rasmi kwa ajili ya semina
kutoka kwa watu ambao wanafanya vizuri kwenye ujasiriamali ambapo itawahusu
wanafunzi wa ngazi ya cheti, diploma na degree ambao ili kuwaandaa kukabiliana
na soko la ajira pindi wanapomaliza masomo yao.
Kilele cha maadhimisho hayo ni siku ya alhamis ya
tarehe 12 May, 2016 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan.
Wiki ya Ujuzi ndani ya Taasisi ya ustawi wa jamii,
inaletwa kwenu kwa kushirikiana na wizara ya elimu kupitia ISWOSO, Social work
club, Human Resource Club, Industrial Relations Club, PSPF na Brighter Monday Tanzania.
Nyote mnakaribishwa.
No comments:
Post a Comment