Viongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi
wa jamii – ISWOSO wameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo
yanayozunguka chuo hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya ujuzi
chuoni hapo.
Pichani ni baadhi ya viongozi walioshiriki katika zoezi la usafi
Zoezi hilo la usafi limeongozwa na wizara ya afya na
mazingira ya serikali ya wanafunzi, na kuwashirikisha pia viongozi wa klabu za
wanafunzi chuoni hapo, ikiwemo klabu ya rasilimali watu (Human Resource),
Mahusiano Kazini (Industrial Relations), na ya uswawi wa jamii (Social Work
Club).
Pichani juu ni baadhi ya viongozi walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi, ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya ujuzi (Career day) ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa siku ya alhamis ya tarehe 12/05/2016 katika viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii.
Siku ya kesho jumatano ya tarehe 11/05/2016,
kutakuwa na semina elekezi kwa wanachuo wanaotarajiwa kumaliza masomo yao
mapema mwezi wa nane mwaka huu, itakayofanyika katika chuo cha ustawi wa jamii.
Semina hiyo imeandaliwa na ISWOSO lengo likiwa ni
kutoa fursa kwa wahitimu ngazi mbalimbali kupata mawazo ya namna ya kutambua
fursa za ajira zilizopo, ambapo wawezeshaji ni kutoka mfuko wa Mafao wa PSPF,
Forever Living, Brighter Monday pamoja na mhamasishaji Chris Mauki na
inatarajiwa kuanza saa saba hadi saa kumi jioni.
Shukrani kwa wapiga picha wote na wote walioshiriki katika zoezi la usafi.
No comments:
Post a Comment