Katika kunogesha maadhimisho ya siku ya ujuzi (Career day)
yaliyofanyika jana alhamisi ya tarehe 12/05/2016, vikundi mbalimbali vya
kitaaluma vilitoa burudani inayohusiana na kile wanachojifunza katika taaluma
yao.
Kwa upande wa taaluma ya Social work, wanaharakati wa kikundi
cha Protect Her 4 Life, chenye lengo la kupambana na kila aina ya ukatili
wanaofanyiwa wanawake na wasichana, kilitoa igizo lililolenga namna ukatili
unavyofanyika, ni kwa kiasi gani kutojielewa au kutojengewa uwezo
kunavyosababisha mtu kutoweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za
kimaendeleo, namna mwanamume anayomtupia lawama mke kwa kila tatizo linalomkuta
mtoto na kuelimishwa kuwa naye anapaswa kuwa sehemu ya kutoa malezi bora kwa
watoto.
Pia igizo hilo lilionesha ni kwa namna gani afisa ustawi wa jamii anavyoweza
kufanya kazi na timu ya wataalamu wa fani mbalimbali, na katika igizo hili
wameshirikiana na polisi kufanikisha mwanamume aliyefanya ukatili amekamatwa na
kufikishwa dawati la jinsia, pia afisa ustawi wa jamii ameweza kushirikiana na
mwalimu wa shule katika kusaidiana kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana hasa
kipindi cha balehe ili kuepuka mimba wakiwa mashuleni na kuonesha ni kwa kiasi
gani maafisa ustawi wa jamii wahahitajika mashuleni. Na pia kumjengea uwezo
mwanamke afahamu haki zake na fursa mbalimbali za kimaendeleo.
Wanachuo wa fani ya ustawi wakijiandaa kwa igizo
Mwanamke aliyepigwa na mumewe akishauriwa kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi, kutokana na kipigo cha mara kwa mara anachokipata kwa mumewe.
Msoma risala kwa upande wa Industrial Relations wao hawakuwa na igizo.