Wanachuo wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo, leo wamejitokeza katika viunga vya eneo la Taasisi hiyo kuchangia damu salama kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Naibu Waziri wa Afya na Mazingira katika serikali ya wanafunzi - ISWOSO Mheshimiwa Judith Mangowi, akiongoza zoezi hilo kwa kuhamasisha wanachuo kushiriki kuchangia damu salama.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Taasisi ya Ustawi wa Jamii - ISWOSO, Mheshimiwa Hemed Haroub, akiteta jambo na mmoja wa wafanyakazi wa Sinza Hospital waliofika kwa ajili ya kuendesha zoezi la uchangiaji na ukusanyaji damu salama katika Taasisi hiyo.
Zoezi la kukusanya damu salama limeendeshwa na Hospitali ya Sinza - Dar es salaam, lengo likiwa ni kuwasaidia ndugu zetu wagonjwa wenye uhitaji wa msaada huu.
ISWOSO, Sinza Hospital na Taasisi ya Ustawi wa Jamii, inatoa shukrani kwa wote waliojitokeza katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment