Saturday, 9 January 2016

PETER MAYUNGA Rais wa serikali ya wanafunzi CBE - MWENYEKITI MPYA WA BARAZA LA SENATE -TAHLISO

Share it Please

 Hatimaye Mwenyekiti mpya atakayeongoza baraza la senate la Jamii ya Vyuo vya Elimu ya juu nchini - TAHLISO apatikana.


Mwenyekiti mpya wa baraza la seneti la TAHLISO akitaka shukran kwa wajumbe wa baraza hilo, baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo.

Mwenyekiti huyo amepatikana baada ya uchaguzi wa mkuu uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ustawi wa jamii kurudiwa kwa mara ya pili na Mheshimiwa Mayunga kuongoza kwa asilimia 60.42 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo cha Diplomasia Mheshimiwa Nice Munissy, aliyepata asilimia 39.58 ya kura zote.

Mheshimiwa Nice Munissy,  mwanamke pekee aliyejitokeza katika kinyang'anyiro cha nafasi ya uenyekiti wa baraza la seneti, akitaka shukrani kwa wajumbe wa baraza hilo, na kuahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa baraza hilo.

Awali wagombea katika nafasi hiyo ya uenyekiti wa baraza la senate walikuwa ni marais saba wa serikali za wanafunzi na zoezi la kuomba kura kwa wajumbe lilitangulia kabla ya uchaguzi kufanyika.

Waliogombea nafasi hiyo ni 

1. Nice Munissy - Rais chuo cha Diplomasia
2. Marwa Wambura - Cardinal Rugambwa Memorial University College - CARUMUCO
3. Eliah Kandonga - Rais Cuhas Bugando
4. Peter Mayunga - Rais wa Chuo cha CBE Dar es salaam
5. Samwel Nyangi - Rais chuo cha Tengeru Institute of Community Development
6. Ernest Kova - Dar es salam Institute of Technology
7. Sylilo Joseph - MUST

Aidha kutokana na kutokuwa na mgombea aliyepata kura zaidi ya asilimia hamsini,  uchaguzi huo ilibidi urudiwe kwa wagombea wawili waliopata kura zaidi ya asilimia kumi na tano, ambao ni Nice Munisy na Peter Mayunga.

Baada ya zoezi la upigaji kura Mheshimiwa Peter Mayunga ndiyo akaibuka mshindi wa nafasi hiyo ya uenyekiti wa baraza la senate TAHLISO kwa kupata asilimia 60.42 ya kura zote.

Wajumbe wa tume ya uchaguzi wakila kiapo kwa pamoja kabla ya kusimamia zoezi la upigaji kura.

Zoezi la kuhesabu kura likiendeshwa kwa umakini

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na wajumbe wake wakitangaza matokeo ya uchaguzi huo.




Baada ya zoezi la uchaguzi wa mwenyekiti wa baraza la seneti - TAHLISO kumalizika, mwenyekiti wa TAHLISO Mheshimiwa Stanslaus Peter Kadugalize, alitangaza majina ya makamishna wakaoongoza idara zilizomo ndani ya TAHLISO.

Makamisha walioteuliwa na nyadhifa zao katika serikali za wanafunzi na vyuo wanavyotoka ni kama ifuatavyo.

Idara ya Mitaala na Taaluma itaongozwa na kamishna Peninna Moka (Spika - Kampala International University) akisaidiana na Kassim Salim Abdi kutoka Zanzibar.

Idara ya Mikopo, Udahili na Usajili itaongozwa na kamishna Godfrey Martin Joho (Rais wa serikali ya wanafunzi - Tanzania  Institute of Accountancy - DSM)  akisaidiana na Japhet Masatu (Rais wa serikali ya wanafunzi Open University of Tanzania - Kinondoni DSM).

Idara ya Habari na Mawasiliano - Kamishna wake ni Hemed Haroub (Rais  Institute of Social Work - DSM), akisaidiana na Aivan Maganza (Rais wa serikali ya wanafunzi St. Joseph University - DAR).

Idara ya Michezo na Ziara mbalimbali - Kamishna wake ni Mkumbo Iman (Rais wa serikali ya wanafunzi Institute of Accountancy Arusha - IAA) na George Albert Mnali (Rais wa serikali ya wanafunzi - Dar es salaam Maritime Institute).

Idara ya Mahusiano, Mihadhara na Makongamano - Kamishna wake ni Thomas Jackson Shauri (Rais wa serikali ya wanafunzi - Hubert Kairuki Memorial University) akisaidiana na Mende Tito (Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi STEMMUCO - Mtwara).

Idara ya Mahafali na Maafa - Kamishna wake ni Neema Lelisha (Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi ST. John Dodoma) akisaidiana na Manusura Lusigaliye (Rais wa serikali ya wanafunzi CBE - Lake Zone).

Idara ya Uchumi - itaongozwa na Kamishna Asha Feruzi (Spika wa bunge la serikali ya wanafunzi - Institute of Adult Education) akisaidiana na Marwa Charles (Rais wa serikali ya wanafunzi - Jordan University - Morogoro).











Wajumbe wa baraza la Seneti - TAHLISO kwa wakifuatilia kwa umakini mkutano wa baraza hilo.





No comments:

Post a Comment

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia