Baraza kuu la viongozi wa serikali ya wanafunzi ya vyuo vikuu nchini, Tanzania Higher Learning Institute Students Organisation - TAHLISO, linalohusisha marais wa vyuo, limekutana katika chuo cha ustawi wa jamii, kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Taasisi hiyo.
Viongozi wanaowakikisha serikali za wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini, waliohudhuria mkutano huo wa uchaguzi.
Kabla ya uchaguzi, mkutano huo ulianza kwa kuwapata wajumbe wa tume ya uchaguzi watakaosimamia uchaguzi huo.
Wajumbe wa tume ya uchaguzi, wakila kipo cha kusimamia uchaguzi kwa uadilifu.
Mkutano huo umehudhuriwa na marais wanaoongoza serikali za wanafunzi kutoka vyuo thelathini na sita (36) Tanzania Bara na Visiwani.
No comments:
Post a Comment