Wednesday, 25 November 2015

MKUTANO WA KWANZA WA SERIKALI YA WANAFUNZI ISWOSO

Mkutano wa kwanza wa wanafunzi ISWOSO - STUDENTS GENERAL MEETING  ( SGM), unafanyika leo katika ukumbi wa chuo lengo kuu likiwa ni uzinduzi  wa katiba mpya ya serikali ya wanafunzi, pamoja na mashindano ya kitaaluma. 

Meza kuu

Katibu mkuu ofisi ya Rais - ISWOSO Mh.Victor Mutalemwa akitaka ufafanuzi wa vifungu vilivyoongezwa katika katiba mpya ya serikali ya wanafunzi.



Wanachuo wakifuatilia hotuba ya Rais akiwasilisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi aliyoiahidi.
Continue Reading...

Monday, 23 November 2015

WELCOME FIRST YEAR FOR NEW INTAKE


Wizara ya Michezo na Burudani ISWOSO imeandaa bash ya aina yake kwa ajili ya kuwa kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza.

Karibu tujumuike pamoja kuwakaribisha wanachuo wenzetu. 
Continue Reading...

Thursday, 19 November 2015

MABORESHO YA VIMBWETA ISW 2015/2016 KUWEZESHA WANAFUNZI KUPATA MAHALI PA KUJISOMEA NYAKATI ZOTE

Katika kuendana na kasi ya mabadiliko katika suala la elimu vyuoni, uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha ustawi wa jamii ISWOSO, kupitia wizara yake ya miundombinu imejipanga kufanya maboresho ya sehemu ya wanafunzi kujisomea (Vimbweta), kwa kuongeza idadi ili viweze kuongeza nafasi zaidi ya wanafunzi kupata sehemu za kujisomea.



Pichani ni Waziri wa Miundombinu ISWOSO 2016/2016 Mh. Erasto Nassary, akionesha sehemu ya vitendea kazi vinavyoendea kutengenezwa kwa ajili ya ujenzi wa vimbweta vipya. (picha zote ni kwa hisani ya wizara ya habari ISWOSO)

Ili kufanikisha suala hilo, wizara ya miundombinu katika serikali ya wanafunzi ISWOSO 2015/2016, imejipanga kuongeza idadi ya vimbweta zaidi ya ishirini baada ya jitihada za kupata ufadhili wa kufanikisha suala hilo kutoka asasi mbalimbali, huku kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL ikitoa mchango wake wa miamvuli 70 iliyoanza kuwekwa kwenye vimbweta vya awali ili wanafunzi waweze kujikinga na jua.




Pichani ni fundi akiendelea na maandalizi ya utengenezaji wa vimbweta vipya. 


Pichani juu ni baadhi ya vimbweta vya zamani vikiwa vimewekwa miamvuli iliyotolewa na Zantel kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kujikinga kipindi cha jua na manyunyu wakati wakijisomea.

Waziri wa Miundombinu ISWOSO 2015/2016 Mh. Nassary akiwa kwenye moja ya vimbweta vya awali vilivyowekwa miamvuli kwa hisani ya kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL.

Mh. Nassari, amebainisha kuwa vimbweta vinavyotarajiwa kutengenezwa vitakuwa kwa mtindo wa duara ili kuendana na sawa na umbo la miamvuli hiyo, na amewataka wanafunzi kutoondoa miamvuli hiyo sehemu ilipo na endapo atakaa kwenye kimbweta ambacho hakina mwamvuli afike ofisi za ISWOSO na kuelezea suala hilo kwani miamvuli mingine imehifadhiwa ofisini na si kuhamisha iliyowekwa kwenye vimbweta vingine.


NB: Shukran kwa kampuni ya Mawasiliano ya ZANTEL kwa msaada wa miamvuli

Continue Reading...

Wednesday, 18 November 2015

VIONGOZI WA KIMILA WAPITISHA AZIMIO LA KUMLINDA MTOTO WA KIKE


Pichani  ni baahi ya viongozi wa kimila (Laigwanan na Laiboni) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan) wilayani Loliondo wakisoma na kujadili azimio la pamoja la kumlinda mtoto wa kila kabla ya kulipitisha na kusaini

Viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai na wanawake mashuhuri wilayani Ngorongoro, wamepitisha azimio la Loliondo lenye lengo la kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha maendeleo yake kiafya, kielimu na kiutamaduni.

Azimio hilo limetiwa sain na viongozi wa hao kwa hitimisho la kongomanao la siku mbili lililofanyika katika ofisi za halmashauri ya wilaya Ngorongoro, lililokuwa na lengo la kupinga mila na desturi zinazomkandamiza mtoto wa kike.

kabla ya kupitishwa na kusaini maazimio hayo, viongozi hao wakimila walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuendeleza mijadala na uelewa wa baadhi ya mila la desturi zinazochangia na kuchochea athari za kiafya na kijamii hasa kwa watoto wa kike na kina mama.

viongozi hao wa kimila (Laigwanan na Laibon) na akina mama mashuhuri (Ngaigwanan), kwa pamoja wamesema watatumia nafasi zao kuelimisha jamii juu ya malezi bora ikiwa ni pamoja na mahali salama pa kulala watoto wa kike na wa kiume na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa elimu hasa kwa watoto wa kike.

Aidha wameiasa jamii ya kimaasai kuacha kuendelea na vitendo vya kuwaoza watoto wa kike wakiwa bado wadogo na wakati mwingine kuwakatisha masomo na kuwalazimisha kuolewa. 

Viongozi hao wamebainisha kuwa matukio ya vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni vimechangia utoro nyumbani na kwenda kuishi kwa muda kwenye vituo maalum kwa kuogopa kufanyiwa tohara na wamekuwa wakitoroka wapogundua kwamba kuna matukio ya ulemavu na athari nyinginezo za kiafyazinazotokana na ukeketaji na salama yao ni kujitoa katika jamii hiyo na kutafuta hifadhi kwingine.

Pamoja na utiani saini wa Azimio la Loliondo, viongozi hao wameliomba shirika la UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kushirikisha viongozi wengi zaidi, kuendelea kuwasaidia katika majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kuwasaidia uratibu wa shughuli zote za kupinga na unyanyasai wa kijinsia.

Kongamano hilo limeendeshwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi  na Utamaduni (UNESCO) limelenga kutoa elimu ya kuwajengea uwezo wa kugawa majukumu kwa viongozi wa kimila, wanawake mashuhuri, viongozi wa dini, wakunga wa jadi pamoja waandishi wa habari ili kutekeleza vizuri ufuatiliaji wa afya ya uzazi na malezi bora kwa watoto katika jamii ya Kimaasai.
Continue Reading...

Wednesday, 4 November 2015

WANAWAKE WAJAWAZITO MANYONI WANAPOTEZA MAISHA KWA KUFUATA HUDUMA ZA AFYA UMBALI MREFU



IMEBAINIKA kuwa wanawake wajawazito wa Kijiji cha Maweni, wilayani Manyoni, Mkoani Singida wamekuwa wakipoteza maisha yao kutokana na umbali mrefu wanaoutumia kufuata huduma za afya ya uzazi kwa wakunga wa jadi.
Hali hii imetokana na kijiji hicho kutokuwa na kituo cha afya au zahanati kwa kipindi kirefu sasa huku ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho kutokamilika hali inayowalazimu kutembea zaidi ya kilomita kati ya 30 hadi 40 kufuata huduma hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mmoja wa wananchi hao, Joyce Karikawe alisema kwa muda mrefu sasa akina mama wajazito hawana huduma za afya jambo linalowafanya watembee umbali mrefu kutoka katika Kijiji hicho hadi kwenye Hospitali ya misheni ya Kilimatinde umbali wa takribani kilomita zisizopungua 30.
Aidha Karikawe alifafanua kwamba pamoja na kufuata huduma hizo Kilimatinde lakini bado kuna baadhi yao wamekuwa wakienda kujifungulia kwa wakunga wa jadi waliopo kwenye maeneo ya kata hiyo,ambayo hata hivyo hupata matatizo makubwa sana,ikiwemo kupoteza maisha yao.
Kutokana na adha hiyo inayowapata wanawake na wananchi kwa ujumla wa kijiji hicho,Karikawe alibainisha kwamba kumewalazimu kufikia maamuzi ya kujenga zahanati katika Kijiji hicho itakayowawezesha kukabiliana na vifo vya akina mama wajawazito vinavyotokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Naye mkazi wa Kijiji cha Maweni, Jacobo Jacksoni Karikawe alifafanua kuwa tatizo la kukosekana kwa zahanati katika Kijiji hicho ni la muda mrefu tangu nchi ilipopata uhuru wake,lakini kutokana na jitihada za diwani wao waliomchagua mwaka 2010 hadi 2015, aliwaonyesha moyo na kuwatia nguvu hadi wameweza kuinua jengo hilo la zahanati.
SAM_0153.jpg
Jengo la zahanati inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambayo itakapokamilika inatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja.
“Lakini jengo hili bado halijakamilika, jengo hili tunaomba msaada kutoka serikalini kwa sababu kuna akina mama wanatoka umbali wa kilomita 15 hadi 20 wanapata matatizo wengine wanajifungulia njiani”alisisitiza Karikawe.
Hivyo mwanachi huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa kuchaguliwa kutosahau ahadi wanazowaahidi wananchi wakati wa kampeni za auchaguzi ili waweze kurejesha imani kwa serikali na kuonya kwamba kutotekelezwa kwa ahadi kunachangia wananchi kutokuwa na imanai na vyama vya siasa wakati wa kuomba kura.
Kwa upande wake Yustasi Wilsoni Mahajile aliweka bayana kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu imekuwa vigumu kwao kukutana na vidonge Kijijini hapo,zaidi ya kwenda kuvifuata kwenye vijiji jirani cha Mvumi,Kintinku hali inayochangia magonjwa ya milipuko pamoja na idadi kubwa ya wagonjwa kupoteza maisha yao.
“Yaani ukishakosa huduma ya afya ina maana magonjwa ya milipuko yanaweza yakatokea na wallio wengi tunakufa,halafu yaani unapokosa dawa ina maana kwamba unatarajia kifo kwa hivyo ukipata zahanati itakuwa ni kimbilio la kuweza kupata maisha pale”alifafanua. 
Hata hivyo kwa upande wake aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye pia ameshinda katika uchaguzi uliofanyika okt, 25,mwaka huu, Abduli Mwengwa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016 Halmashauri ya wilaya ya Manyoni imetenga zaidi ya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho.
Kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji cha Maweni,Merina Nyambuya alisema ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho ulioanza mwaka 2012 kwa nguvu za wananchi unatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja utakapokamilika na kwamba mpaka sasa lilipofikia hatua ya umaliziaji limetumia zaidi ya shilingi milioni 41.

NB: Shukran Zainul Mzige wa Moblog
Continue Reading...

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia