
Baadhi ya wanachuo wa taaluma ya ustawi wa jamii waliohudhuria maadhimisho hayo

Baadhi ya wanachuo wa taaluma ya Industrial Relation waliohudhuria maadhimisho hayo

Baadhi ya wanachuo wa taaluma ya Human Resource waliohudhuria maadhimisho hayo
Akitoa salamu za ufunguzi, rais wa serikali ya wanafunzi chuo
cha ustawi wa jamii Mheshimiwa Hemed Haroub, amebainisha kuwa siku hii inalenga
kuwakutanisha pamoja wajuzi wa fani zinazotolewa katika chuo cha
ustawi wa jamii, pamoja na wale walio katika ajira, katika kushea mambo
mbalimbali, na pia kutoa mawazo ya fursa za ajira.
Mheshimiwa Hemed - rais wa serikali ya wanafunzi

Rais wa serikali ya wanafunzi Mheshimiwa Hemed Haroub (aliyesimama) akitambulisha meza kuu, wa kwanza kulia ni makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo Mheshimiwa Stella Wadson
Kilele cha maadhimisho hayo kimefana kwa wanachuo
kuainisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na taaluma zao kwa njia ya maelezo,
maigizo na kupitia risala.

Pichani juu ni wanachuo wa taaluma ya ustawi wa jamii, wakielezea mambo mambo mbalimbali wanayofundishwa katika taaluma hiyo na namna inavyowasaidia katika kufanya kazi mbalimbali za kijamii.

Pichani ni wanataaluma ya Industrial Relation wakielezea shughuli zinazotekelezwa na wanataaluma hiyo pamoja na process nzima inavyotakiwa kufuatwa wakati wa kufanya Mediation.

Hapa ni kwenye meza ya wanachuo wa taaluma ya rasilimali watu (Human Resource) nao wakielezea kile wanachokipata katika chuo cha ustawi wa jamii, pamoja na namna taaluma hiyo inavyofanya kazi kwenye soko la ajira.
Wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali waliweza
kuhudhuria katika career day ya ustawi wa jamii, kutoa changamoto mbalimbali
zinazotokana na ajira na pia kutoa mwongozo wa namna ya kuchangamkia fursa
mbalimbali za ajira.
Miongoni mwa mashirika na wadau waliohudhuria ni
pamoja Brighter Monday, PSPF, Zoom Tanzania pamoja na wawakilishi wa vyuo
mbalimbali kikiwemo chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mwakilishi kutoka Brighter Monday, akielezea fursa mbalimbali za ajira zinazopatikana endapo mtu atajiunga online ili kupata taarifa mbalimbali za nafasi za ajira hapa nchini, kutoka kwa mashirika mbalimbali.
Career day katika ustawi wa jamii imeandaliwa na
wizara ya elimu kutoka serikali ya wanafunzi ISWOSO kwa kushirikiana vilabu vya
kila taaluma itolewayo ambapo kwa upande wa Human Resource inafahamika kama
IHUMRESA, Industrial Relations – IRESA na Social Work – SOWOC.
Waziri wa elimu katika serikali ya wanafunzi - ISWOSO Mheshimiwa Mabena, akihojiwa na chombo cha habari cha ITV, kuelezea lengo la career day.

Pichani juu ni baadhi ya wanachuo waliohudhuria kwenye career day, iliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ustawi wa jamii.
Maadhimisho ya career day hufanyika kila mwaka na kwa kipindi yamehusisha taaluma zote tatu zinazotolewa katika chuo cha ustawi wa jamii ambazo ni Social work, Human Resource, na Industrial Relations, lengo likiwa ni kuziweka pamoja na kuongeza ufanisi, kwani hata katika soko la ajira zinategemeana, tofauti na miaka ya nyuma ambapo kila taaluma ilikuwa inaadhisha kivyake.