Tuesday, 18 August 2015

TAHADHARI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR NA WANACHUO : KIPINDUPINDU CHAIBUKA

Share it Please
Ugonjwa wa kipindupindu umelipuka tena jiji ni Dar es salaam.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana Said Meck Sadick  ametoa tahadhari kwa wakazi wa jiji hilo, kuwa makini kwa kuzingatia kanuni za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam bwana Said Meck Sadick

Ugonjwa huo tayari umekwishapoteza maisha ya watu wawili (mwanamke na mwanaume)  kutoka maeneo ya Tandale na Mwananyamala.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa ugonjwa huo umeandika kuwepo wilaya ya Kinondoni kwenye kata za Kijitonyama, Kimara, Tandale na maeneo ya jirani na hayo.

Kutokana na ugonjwa huo wananchi wa meta kuwa kuzingatia suala la usafi wa mwili na mazingira ikiwa ni pamoja na kuepuka kula hivyo na kunawa mikono kila mara ili kujikinga na ugonjwa huo.

Mara ya mwisho ugonjwa wa kipindupindu ulilipuka jiji ni Dar es salaam mwaka 2010 ambapo watu 17 walilazwa wakitokea manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni. 

No comments:

Post a Comment

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia