Viongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO pamoja na wanachuo wengine, wamefanya ziara ya mafunzo kwenye makao makuu ya kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi - Airtel kujionea bidhaa mbalimbali na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
Wanachuo wakielekezwa teknolojia mpya ya huduma kwa wateja ambapo badala ya mteja kupanga foleni na kusubiri kuhudiwa kuhusiana na huduma mbalimbali, kuna computer maalum zimeandaliwa na mteja mwenyewe anaelekezwa namna ya kujihudumia kulingana na huduma anayoihidaji mfano, huduma za Airtel money, vifurushi na huduma nyinginezo.
Airtel pia hutuo fursa za ubunifu kwa vijana na watu wa rika zote kama amebuni teknolojia mpya ambayo anahisi anaweza kushare nao au kuiuza na wakati mwingine kuwa consultancy, anaweza peleka wazo lake na likajadiliwa na team ya Airtel, na ikionekana inamashiko basi mbunifu atapata fursa ya kuingia mkataba na Airtel kuhusiana na huduma hiyo. Hangout ni sehemu maalum ya makutano hayo ya kujadili
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi wakiwa sehemu ya Hangout, kujifunza namna Airtel wanavyowajali wateja wao wa ngazi tofauti (Mwenye shasimu mkononi aliyekaa ni waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi - ISWOSO Mheshimiwa Maurice Bendera na anayetazama kamera mwenye shati jeupe ni waziri wa fedha Mheshimiwa Nyalusi).
Pia wanachuo walipata fursa ya kipekee ya kuelezewa huduma mpya ya kadi ya malipo maarufu kama TAP TAP - Gusa Usepe, ambapo mteja anayetumia huduma ya Airtel money anaweza kutumia kadi hii kwa malipo yake, wakati akinunua bidhaa mbalimbali katika maeneo ambayo huduma hii inafanya kazi badala ya kutembea na fedha mkononi. Kwa kuanzia huduma hii TAP TAP - Gusa Usepe inapikana jijijini Dar es salaa, katika Supermarket ya TSN (moja ya supermarket hiyo ipo jirani na Chuo cha Ustawi wa Jamii), hivyo ni fursa pekee pia kwa wanachuo na wengineo, kutumia huduma hiyo nzuri na ya haraka, na inapatikana hata kama simu yako haina chaji, ili mradi tu, uwe na salio lako la Airtel money, na uwe na kumbukumbu na ya namba yako ya siri.
.
Pichani ni Aina ya kadi ya TAP TAP - Gusa Usepe na inapatikana kwa gharama nafuu sana.
Afisa masoko wa Airtel bwana Prosper, akiwasikiliza wanachuo (hawapo pichani), walipokuwa wakiuliza maswali ya ufafanuzi wa huduma za vifurushi vya chuo.
Mmoja wa vijana waliopata fursa kutoka Airtel ambaye alikuwa ni mwanachuo katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM, akitoa ushuhuda wake kwa wanachuo wenzake namna alivyofanikiwa.
Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha ustawi wa jamii - ISWOSO Mheshimiwa Stella Wadson (kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Abubakar Mvungi wakipata msosi ndani ya Hangout ya Airtel makao makuu - Dar, wakati wa ziara ya mafunzo
Mbali na huduma hizo pia, Airtel kwa sasa imezindua Modem ya kipekee ya wingle na WiFi, ambayo inawezesha wateja wake kufurahia huduma za internet na Wi-Fi kwa pamoja yenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.
Ni wakati wako sasa kujiunga na mtandano wa Airtel wenye huduma nafuu, huduma za kukopa na kulipa kwa gharama nafuu itakayokuwezesha kujikwamua kwa mambo mbalimbali na pia kufaidika na huduma za UNI kwa wanachuo ambayo imeboreshwa na ni gharama nafuu.
AIRTEL - KAMATA FURSA
No comments:
Post a Comment