Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi imeandaa kongamano la saba la elimu juu nchini kuandaa mikakati mbalimbali ya elimu nchini. Wizara imeandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), pamoja na kamati ya wakuu wa vyuo vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
Mwenyekiti wa Tume ya vyuo vitu Tanzania, Profesa Awadh Mawenya, ambaye ni mgeni rasmi katika kongamano la elimu ya juu lililofanyika jijini Arusha akiongea machache mara baada ya Kumaliza kutoa mada.
Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya elimu.
Katibu mtendaji wa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) Profesa Yunus Mgaya akiwashukuru washiriki katika kongamano la saba la elimu ya juu lililofanyika jijini Arusha.
Meza kuu
Profesa Sylvia Temu, mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya juu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi akiongea na vyombo vya habari juu ya mikakati na mipango ya kongamano la saba la elimu ya juu.
Washiriki na kongamano la Elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment