Monday, 12 October 2015

TAMASHA LA MTOTO WA KIKE LAFANA NA LATOA KAULI NZITO


WAKATI serikali imekiri kwamba pamoja na kuwa na sheria kali za kuzuia ukatili kwa watoto bado kuna matukio mengi yanayowanyima watoto uhuru na haki zao msingi,wadau mbalimbali walioshiriki tamasha la mtoto msichana wamewataka wasichana kutimiza ndoto zao.
Katika tamasha hilo lililofanyika katika shule ya msingi Tandale, wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane vipaji mbalimbali vya watoto vilioneshwa na watoto nao kutoa kauli zao za kutaka haki na ustawi wao kwani wao ni taifa la sasa.
DSC_0486.JPG.jpg

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe Mussai akiwaasa watoto wa kike kuzingatia elimu kwani ndio nguzo ya msingi katika maisha yao wakati w siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Tandale jijini Dar.

Pamoja na watoto hao kutoa ushuhuda na kuonesha njia ya kusaidiwa, Mkurugenzi wa watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii , jinsia na watoto Margaret Sawe Mussai pamoja na kuwaambia watoto na jamii kutumia simu 119  kuelezea ukatili, ametaka madawati yaliyopo Polisi kutumika vilivyo kukabiliana na vitendo hivyo.
Alisema lazima wazazi na walezi wawajibike katika kulinda watoto kwani taarifa zilizopo sasa haziridhishi hata kidogo.
Alisema taarifa zilizopo watoto wa kike asilimia 29 na wavulana asilimia 13 wamenyanyaswa kijinsia wakati wasichana asilimia 14 na wavulana asilimia 6 wamekabiliwa na tatizo la kujaribiwa kuvurugwa kijinsia.


DSC_0418.JPG.jpg


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar.

Akizungumzia suala la mimba za utotoni alisema kwamba wizara imeandaa program za kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni huku akisema kwamba sheria ya ndoa ya mwaka 1971 iko mbioni kubadilishwa ili kupandisha umri wa kuolewa kuwa miaka 18.
Aidha alisema serikali na wadau wengine wanaendesha mafunzo ya kuwatoa watoto katika mazingira hatarishi pamoja na kusaidia wazazi vijana ambao walikatisha shule kutokana na ujauzito.
Mkurugenzi huyo pamoja na kueleza changamoto za malezi na ulinzi kwa watoto amesema sera zilizopo zinaendelea kuboreshwa ili kutoa ulinzi zaidi katika kuhakikisha taifa linakua na watoto wenye uhakika wa usalama.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu UNFPA Dk. Natalia Kanem alisema mtoto msichana anahitaji kushikilia ndoto yake pamoja na changamoto zinazojitokeza.
Alisema pamoja na kuwepo kwa vikwazo vya mawasiliano , mtoto wa kike anastahili kupewa taarifa mbalimbali zinazomweka huru katika mambo ambayo yanamhusu yeye na jamii yake.
Alisema pamoja na haja ya kuwepo kwa usawa wa kijinsia, mtoto wa kike ni lazima apate haki yake ya kusoma,kutodhuriwa na utamaduni uliopitwa na wakati ambao ni kandamizi kama kukeketwa na ndoa za utotoni na kutobaguliwa.

DSC_0309.JPG.jpg


Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisoma risala kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale jijini Dar

Aliwataka watoto wa kike kuhakikisha kwamba wanasoma kwa kuwa elimu ni kila kitu na wakishakuwa na elimu watajiamini na kujitambua.
Alisema ipo haja ya kuimarisha mfumo wa ulinzi kwa watoto wa kike ili  kupata nafasi ya kusonga mbele na wale ambao wamekatishwa masomo kwa sababu mbalimbali kurejea darasani ili kupata elimu na uwezo wa kuendelea mbele.
Alisema kw akuunganisha nguvu kati ya serikali, mashirika ya umoja wa mataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo na mtoto wa kike,watoto wa kike watapata nafasi kubwa ya kusonge mbele.
Aliwataka watoto wa kike kujitambua kwamba wao ni wazuri lakini wanapaswa kujiheshimu na kuwaheshimu wengine kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo yao.
“Wale wanaoapata mimba, wale wanaokatishwa masomo ni lazima wapate njia ya kujiendeleza tena” alisema Dk Natalia.
DSC_0343.JPG.jpg

Angel Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani akieleza alipotokea mpaka kufika alipo sasa wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika siku ya Jumamosi.
Katika tamasha hilo wasichana wawili walitoa ushuhuda, Binti mdogo Eva Tolage ambaye alimwandikia barua Rais Barak Obama akihoji Marekani na yeye binafsi rais Obama na viongozi wa dunia watafanya nini kumsaidia mtoto wa kike anayekabiliwa na changamoto nyingi hasa wale wa vijijini.
Eva alimwambia Barack Obama kwamba anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa askari kusaidia jamii, lakini atafikiaje ndoto hiyo wakati kuna changamoto ya umeme na huku baba yake kazi anazofanya hazimpi kipato cha kutosha.
Msichana huyo ambaye aliandika barua kwa ujasiri mkubwa akihoji maendeleo endelevu yasiyompita binti mdogo alijibiwa na Rais Obama na kutajwa katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa kwamba viongozi wa dunia akiwemo Barack Obama mwenyewe wamemsikia na watahakikisha tatizo la wasichana wa Afrika na kwingine kokote linaondolewa na na wanapata nafasi ya kushiriki katika maendeleo.
DSC_0362.JPG.jpg

Eva Tolage aliyeandika barua kwa rais Barack Obama wa Marekani na barua yake kusomwa katika mkutano wa viongozi wa dunia makao makuu ya Umoja wa Mataifa alitumia mkutano huo kusoma machache aliyoandika. Katika barua hiyo, Eva mwenye umri wa miaka 15, alielezea jinsi ambavyo bado mazingira mtoto ni mabovu na hatarishi kiasi cha kumfanya ashindwe kupata elimu bora, pia kuwa katika hatari ya kukumbwa na vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Aidha binti mwingine Angela Benedicto ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wote sawa alisimulia  matatizo ya wasichana wa kazi,adha zao kutoka kwa wanaume na watoto wa kiume wanakofanyia kazi.
Alisema kwamba mateso wanayoyapata wasichana wa kazi yanastahili kukoma na kwamba ipo haja ya kuwekwa kwa mfumo unawalinda.
Alisema serikali ina wajibu wa kuwatetea wasichana kupata haki zao, sio tu kusema shule bure, lakini pia kujenga kujiamini kwa wasichana katika kutimiza ndoto zao.
Alisema sababu za kuwepo kwa wasichana wengi wakazi za ndani ni dhuluma inayoambatana na umaskini katika familia na tamaduni zinazomweka nyuma mtoto wa kike kiasi cha kulazimika kutafuta kazi za ndani ambazo waajiri wanakuwa hawana staha.
Katika tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za kuangalia hali ya afya ya uzazi, elimu ya afya ya uzazi, kupimwa maambukizi ya UKIMWI na kukaguliwa kwa saratani ya matiti na kizazi pamoja na elimu yake.
Pia kulikuwa na michezo ya kuigiza na sarakasi na mwanamuziki wa kike mwasiti alichombeza kwa nyimbo zake za uadilifu.
Siku ya Mssichana duniani huadhimkishwa Oktoba 11 lakini kwa Tanzania iliadhimishwa Oktoba 10.

DSC_0751.JPG.jpg

Mgeni rasmi pamoja na vingozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wenye ulemavu wa ngozi katoka maadhimisho ya siku wa mtoto wa kike.
DSC_0750.JPG.jpg


Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe Mussai (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem ( wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na watoa huduma katika mabanda yaliyokuwepo kwenye maadhimisho hayo.


Continue Reading...

Friday, 9 October 2015

Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kufanyika Octoba 13 viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar


Kila Oktoba 24 ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kuundwa kwake. Kwa mwaka huu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yanayofanya kazi kama taasisi moja yameendelea kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo.

Akizungumza  na waandishi wa habari Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez kuhusu  umuhimu wa  malengo hayo  amesema “Kwa hakika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni wito wa kujitazama, kuona yale tuliyofanya kwa miongo kadhaa na kujikita kuona namna  ya kuabiliana na umaskini hapa nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla
DSC_0162.JPG.jpg

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.
DSC_0181.jpg

Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa  kwa Umoja wa Mataifa yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
“Malengo ya Maendeleo endelevu ni wito wa kuwajibika kwetu sote.  Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake.  Inabidi tufanye kazi kwa pamoja,wadau wote,serikali na bunge, vyama vya kiraia, madhehebu ya kidini, wafanya biashara, wajasiliamali, na wanazuoni.Na hakika tukishirikiana kwa nguvu pamoja na amani tunaweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu”
Pia alisistiza kuwa “Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumzana waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya amesema kuwa nia ya serikali ni kuendelea kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na kuwatakawatengeneze sera nzuri ambazio zitahakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mipango ya maendeleo ya kitaifa.
DSC_0174.JPG.jpg
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni.

Aliendelea kufafanua kwa kusema Tanzania inafurahishwa na ukweli unaoonekana kwenye malengo mapya ya maendeleo endelevu kwani  yamechota pia yale malengo ya milenia ambayo yalikuwa bado hayajamaliziwa kwani katika hayo kunaweza kuleta mabadiliko ya kuwezesha kuondokanana umaskini katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya Umoja wa mataifa yatafavyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam siku ya Jumanne Oktoba 13 badala ya siku iliyozoelekaya Oktoba 24 ili kupisha uchaguzi mkuu wa  Tanzania unaofanyika Oktoba 25. Na kauli mbiu ya maadhimisho ya Umoja wa mataifa mwaka huu ni “Umoja wa Mataifa uliothabiti, Dunia bora”.
DSC_0048.JPG.jpg

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0071.JPG.jpg

Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo namba 4 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0023.JPG.jpg

Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wameshikilia lengo namba 5 na 10 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0085.JPG.jpg

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiwa ameshikilia lengo namba 17 kati ya  malengo 17  ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
DSC_0120.JPG.jpg

Afisa Habari wa Shirika la kazi duniani (ILO)  Tanzania, Magnus Minja na Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakiwakilisha lengo namba 1 na 8.

NB: Shukran Pamoja Blog na Mo Blog kwa kufanikisha habari hii.


Continue Reading...

Thursday, 8 October 2015

TAHADHARI YATOLEWA KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA ANTIBIOTIKI BILA USHAURI WA DAKTARI


Juhudi zaidi zinahitajika  na utashi wa kisiasa katika  kudhibiti usugu wa dawa za antibiotiki ili isije ikafikia mahali ambapo  dawa hizo zikakosekana katika kutibu magonjwa ya kuambukiza, pia wito umetolewa kwa jamii  kuwa na matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki ili kuweza kupunguza usugu wa dawa hizo.
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Antibiotic Resistance  Partnership (GARP), Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba Shirikishi( MUHAS) wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia kuhusu matumizi na usugu wa dawa za Antibiotikiya mwaka 2015,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambapo alisema ripoti hiyo imetoa mapendekezo hayo.


1412.jpg

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari (kushoto wa pili) akizindua ripoti ya dunia kuhusu matumizi na usugu wa dawa za Antibiotiki ya mwaka 2015, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa Antibiotic Resistance Partnership (GARP), Profesa Said Aboud kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi za Tiba Shirikishi (MUHAS) na kulia wa pili ni Makamu Mwenyekiti wa wa Antibiotic Resistance Partnership (GARP), Profesa  Robinson Mdegela kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na kulia wa pili ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Henry Irunde.


Aidha tatizo la usugu wa dawa hizo linachangiwa na kutokuwepo kwa usimamizi madhubuti katika kununua dawa kutoka katika maduka ya dawa bila cheti cha daktari.
 Akizungumzia kuhusu suala hilo, Profesa Aboud alisema  Watafiti wa Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Magonjwa, Uchumi, na Sera(Center for Disease Dynamics,Economics & Policy(CDDEP) )wakishirikiana na nchi washiriki ikiwemo Tanzania walitoa ripoti mpya inayoonesha kiwango kikubwa cha usugu wa dawa hizo zinazotumika kutibu magonjwanya kuambukiza ambayo yanapelekea kuhatarisha maisha ya watu dunia.
Alisema ripotoi hiyo ilizinduliwa Septemba 17,mwaka 2015 mjini Washington,Marekani inaonyesha usugu na matumizi yasiyosahihi ya dawa za antibiotiki na mipango ya kitaifa inayotumika katika kupambana na tatizo hilo.
“The State of the World’s Antibiotics 2015 ni ripoti ya kwanza kuonyesha kwa kina ukubwa wa tatizo la usugu wa dawa za antibiotiki kidunia kwa binadamu, wanyama na mazingira. Ripoti hiyo imetoa mikakati mipya ambayo kila nchi ikiwemo Tanzania ionapendekezwa kuifanyia kazi ya kupambana na tatizo hilo linaloenea kwa kwa kasi.
“Ripoti hiyo inaonyesha kuwa matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki kutibu magonjwa ya kuambukiza ni mojawapo  ya njia muhimu kupambana na usugu wa dawa za antibiotiki na hili  likiwezekana litaondosha dhana kuwea suluhisho la usugu wa dawa za antibiotiki ni kukosekana kwa dawa mpya za antibiotiki za kutibu magonjwa ya kuambukiza ,” alisema Profesa Aboud.
Aliongeza  kwamba nchi tajiri duniani zinatumia dawa za antibiotiki kwa kiasi kikubwa ,tatizo la usugu wa dawa za antibiotiki kwa nchi masikini na zenye uchumi wa kati ni kubwa duniani linahitaji juhudi za makusudi kupambana nalo.
Profesa Aboud alisema tafiti zilizofanyika Tanzania zinaoyesha kuwa kuna kiwango kikubwa cha usugu kwa dawa za antibiotiki kwa bakteria aina ya Streptococcus pneumonia anayesababisha homa ya mapafu kwa watoto. Magonjwa ya kifua pamoja na homa ya mapafu yanasababisha kwa asilimia 15 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano katika mwaka 2013 na Watanzania 35,000 walikufa kwa homa ya mapafu mwaka 2012 kutokana na bacteria sugu aina ya Streptococcus pneumonia.
 Alifafanua kwamba usugu wa dawa hizo umeonekana katika vinyememea vya maradhi vya bacteria katika uambukizo wa njia ya mkojo,kisonono na kaswende katika miaka 15 iliyopita.
“ Kama hali ya usugu wa dawa za antibiotiki itaachwa kuendelea ,magonjwa Ya kisonono na kaswende hayatatibika na kusababisha ugumba na upofu wa watoto wa change wanaozaliwa,” alisisitiza.
 Alisema kwa mara ya kwanza ripoti hiyo inaonyesha taarifa kutoka nchi masikini kama Tanzania na zenye uchumi wa kati ambapo tatizo la usugu wa dawa za antibiotiki ni kubwa lakini haionyeshi juhudi za makusudi zikichukuliwa kupambana na tatizo hilo.
Ripoti hiyo imetumia uzoefu uliopatikana kutoka nchi nane katika Afrika ikiwemo Tanzania na Asia kupitia mradi wake wa kimataifa wa kupambana na usgu wa dawa za antibiotiki(Global  Antibiotiki Resistance  Partnership(GARP).
 Alizitaja njia nyingine ambazo zimetolewa kama mapendekezo yanayowezakutumika kupambana na tatizo hilo kuwa ni kuwa na kampeni ya matumizi sahihi ya dawa hizo kutibu magonjwa ya kuambukiza, kudhibiti magonjwa ya kuambukiza katika hospitali, kutoa  chanjo kukinga magonjwa ya kuambukiza na kupunguza matumizi ya antibiotiki yasiyo ya lazima ya lazima kutibu magonjwa ya kuambukiza, ikiwemo na utoaji wa elimu kwa umma.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari alisema Serikali imeyapokea mapendekezo ya ripoti hiyo, hivyo wizara yake itatoa miongozo juu ya suala hilo baada ya kujadiliana na wataalamu mbalimbali.
109.jpg

Picha ya pamoja kati ya Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari na wadau wa uzinduzi huo.


NB: Shukran Idara ya Habari Maelezo na Mo Blog kwa habari hii.

Continue Reading...

Tuesday, 6 October 2015

Top Jobs Kutoka Brightermonday wiki hii - Tembelea huku kwa ajira mbalimbali


vacancies.jpg
Access Bank Tanzania – NAFASI 1 – http://bit.ly/1VcFaMV

 
Kilimanjaro Christian Medical University College – NAFASI 1- http://bit.ly/1jJQeQL
 
International Organization for Migration (IOM) – NAFASI 3- http://bit.ly/1VABAHs
 
Emerson Education – NAFASI 2- http://bit.ly/1M5M4cw
 
utrack Africa Limited – NAFASI 1 – http://bit.ly/1RqwkFJ
 
Internews TZ – NAFASI 1 – http://bit.ly/1VyFTYV
 
Public Service Recruitment Secretariat – NAFASI 16 – http://bit.ly/1iYYtI1
 
Favorite HR Services – NAFASI 8 – http://bit.ly/1VyHdLw
 
RK Impact Consulting (RK Consulting) – NAFASI 2 – http://bit.ly/1L1xfIk
 
African Development Bank Group – NAFASI 8 – http://bit.ly/1Of1YG5
 
Voluntary Service Overseas (VSO) Tanzania – NAFASI 2 – http://bit.ly/1NgcDlt
 
Nobeah Foundation  – NAFASI 55 – http://bit.ly/1MTZnzS
 
Winning Spirit High School – NAFASI 1 – http://bit.ly/1JOmE1x
 
Workforce Management & Consultancy Ltd – NAFASI 1- http://bit.ly/1Q0uYAu
 
Institute of Adult Education – NAFASI 7 – http://bit.ly/1QU90iG
 
Muhimbili University of Health and Allied Sciences – NAFASI 1 – http://bit.ly/1VAJ8Kf
 
UNESCO National Commission-Tanzania – NAFASI 6  – http://bit.ly/1VAJlwN
 
Sra-Technologies – NAFASI 2 – http://bit.ly/1Ngejv0
 
Dangote Industries Limited, Tanzania – NAFASI 2 – http://bit.ly/1VAJSz5
 
Stamigold –  NAFASI 4 – http://bit.ly/1Q0wGSq
 
KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI KUHUSU MASUALA YA KAZI;
Facebook: Brightermondaytz
Instagram: @Brightermondaytz
Continue Reading...

Friday, 2 October 2015

KONGAMANO LA SABA LA ELIMU YA JUU LAENDELEA JIJINI ARUSHA

Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi imeandaa kongamano la saba la elimu juu nchini kuandaa mikakati mbalimbali ya elimu nchini. Wizara imeandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), pamoja na kamati ya wakuu wa vyuo vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho. 

Mwenyekiti wa Tume ya vyuo vitu Tanzania, Profesa Awadh Mawenya,  ambaye ni mgeni rasmi katika kongamano la elimu ya juu lililofanyika jijini Arusha akiongea machache mara baada ya Kumaliza kutoa mada.

Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya elimu.

Katibu mtendaji wa Tume  ya vyuo vikuu nchini (TCU) Profesa Yunus Mgaya akiwashukuru washiriki katika kongamano la saba la elimu ya juu lililofanyika jijini Arusha.

Meza kuu

Profesa Sylvia Temu, mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya juu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi akiongea na vyombo vya habari juu ya mikakati na mipango ya kongamano la saba la elimu ya juu.




Washiriki na kongamano la Elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

Continue Reading...

Thursday, 1 October 2015

International Day of Older Persons - Sustainable Cities for All Ages

UNFPAs-Executive-Director-Dr.-Babatunde-Osotimehin..jpg
UNFPA’s Executive Director, Dr. Babatunde Osotimehin.



Statement on the International Day of Older Persons by Dr. Babatunde Osotimehin, UNFPA Executive Director.
Population ageing and urbanization are major global issues of the 21st century. While cities are growing, their share of residents aged 60 years and over is also rising. Rapid urbanization is challenging both national and local governments in developing inclusive and integrated cities.
Today, as we observe the International Day of Older Persons, we must ensure that cities respond to the needs of persons of all ages and that older persons are as much a part of urban life as their younger counterparts.
This year’s theme of Sustainability and Age Inclusiveness in the Urban Environment fits in perfectly with the objectives of the recently adopted 2030 Agenda for Sustainable Development: leave no one behind! Together, we must ensure that older persons are fully integrated in cities’ economic, social, political and cultural life.
What can we do to make our cities more inclusive? We can start by ensuring that both younger and older generations are included in the urban planning process and their issues, needs and concerns are equally taken into account.
We need an approach to urban planning that focuses on well-being throughout the life cycle. We should invest in young people today by promoting healthy habits, ensuring education and jobs, and providing access to health services and social security coverage for all workers. This is the best investment to improve the lives of young people, help stem the increasing tide of out-migration, and improve the lives of future generations of older persons.
At the same time, we must provide affordable and accessible health-care services, lifelong learning and retraining opportunities, and flexible employment for older persons to improve their well-being and facilitate their integration into the fabric of communities.
Strengthening human capital by ensuring empowerment, education and employment of all citizens will yield a high return on investment and will help countries reap a demographic dividend that can lift millions out of poverty. Creating hope and opportunity for young people to develop their full potential can drive progress in the years to come and, ultimately, result in a second demographic dividend of healthier, wealthier and more productive older persons.
Today, we call on policymakers and urban planners to work together to ensure an inclusive urban environment for all ages. This means paying particular attention to the important pillars of urban living, such as housing, transportation, basic social services, and health care, to make them age-friendly. It means creating an ageless society, characterized by an urban physical environment that facilitates personal mobility, safety and security. It means creating an urban social environment that encourages respect, social inclusion, and participation. And it means protecting natural resources, preparing for natural disasters, and reducing risk so that current and future generations look forward to a sustainable future.
Today, we call on urban leaders to ensure the protection of the human rights of all urban residents, including the elderly who are more vulnerable, and to enforce zero tolerance of discrimination, neglect, violence and abuse of older persons.
Ensuring sustainability and age inclusiveness in the urban environment means creating a society for all ages where the voices of all generations are heard and where the needs of both young and old are met. It means empowering young and old to fully participate in the economic, social and political life of their communities. It means gathering data on city residents and their needs and working to ensure that they are adequately met. It also means sharing experiences about what makes a city a great place to live in for both young and old.
Age-friendly cities are not just elderly-friendly. They are better for everyone.

Continue Reading...

Followers

Check us on Facebook

Designed By WijasWillie | SharpMedia